Hits 86460 | 4 online
MKURUGENZI SERA MIPANGO NA UTAFITI BI DAIMA .M. MKALIMOTO
MKURUGENZI SERA MIPANGO NA UTAFITI BI DAIMA .M.MKALIMOTO
Wizara imeendelea na jukumu lake la kuratibu na kusimamia utekelezaji wa miongozo mbalimbali ikiwemo sera, sheria na kanuni ambapo kwa kipindi hiki imekamilisha matayarisho ya kuanzishwa kwa Jukwaa la pamoja la wadau wa sekta ya sheria (JSF), imeandaa rasimu ya Sera ya Skuli ya Sheria na kuitafsiri kwa lugha ya Kiswahili. Ni imani yetu kwamba sera hii itatoa muongozo madhubuti wa uendeshaji wa Skuli ya Sheria Zanzibar. Kazi mbili hizi ni mchango kupitia washirika wa maendeleo UNDP chini ya Mradi wa Kuimarisha Uwezeshaji wa Kisheria na Upatikanaji wa Haki (Legal Empowerment and Access to Justice Project - LEAP). Wizara pia imefanya mapitio pamoja na kuandaa Sheria mbalimbali zikiwemo Sheria ya Jumuiya ya Mawakili Zanzibar, Sheria ya Mawakili, Sheria ya Mufti na Sheria ya Skuli ya Sheria.