Head image
Govt. Logo

Hits 70158 |  3 online

     
Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na taasisi zake zote wameadhimisha Wiki ya Sheria kwa kufanya mambo mbalimbali
news phpto

KATIBU MKUU WIZARA YA KATIBA NA SHERIA NDG GEORGE JOSEPH KAZI

KATIBU MKUU NDG GEORGE J. KAZI

Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na taasisi zake zote wameadhimisha Wiki ya Sheria kwa kufanya mambo mbalimbali yakiwemo, uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Mahakama ya Tunguu, kufanya maonesho katika Viwanja vya Mnazimmoja, kuadhimisha wiki ya msaada wa kisheria iliyokwenda sambamba na uzinduzi wa Daftari la msaada wa kisheria ambalo ni Mfumo wa Usajili wa watoa huduma za msaada wa kisheria, kutoa elimu kwa jamii kuhusu taratibu za upatikanaji wa haki pamoja na taasisi zote za kisheria pamoja na wadau wa sekta ya sheria kufanya matembezi ya maadhimisho hayo.

Wizara pia inaendelea kushirikiana vyema na Wizara ya Katiba na Sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, katika kuimarisha ushirikiano na nchi nyengine watendaji na viongozi wa wizara walihudhuria mikutano inayohusu sekta ya sheria nchini Afrika ya kusini, India, Namibia na kushiriki Mkutano wa Vyombo vya Sheria vya Nchi za Asia na Afrika (AALCO). Kwa sasa Wizara ipo katika maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri, Wanasheria Wakuu na Watendaji wa Sekta ya Sheria wa Nchi za SADC, unaotarajiwa kufanyika mwezi Aprili 2020.

Huduma za Tehama

Barua Pepe Msaada wa kisheria

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

MAHAKAMA DPP WAKFU LRC SADC IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 772, Mazizini, Zanzibar
Tel.: +255(24)2234683 Mhe WaziriTel.: +255 (24)2234684 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2234689
Email: info@sheriasmz.go.tz