Head image
Govt. Logo

Hits 70233 |  3 online

Mrajis wa Mahakama Kuu Zanzibar Mhe Mohamed Ali Mohamed akisoma taratibu za kiutawala na dharura za kukinga na kupunguza maambukizi ya virusi vya korona (COVID 19) kwa upande wa Mahakama Zanzibar
news phpto

Kufuatia maelekezo yaliyotolewa na Serikali ya Zanzibar tarehe 17 Machi, 2020 juu ya kujikinga na kupunguza kuenea kwa virusi vya corona (COVID- 19) hapa Zanzibar, natoa muongozo ufuatao katika uendeshaji wa kesi Zanzibar.

1. Usikilizwaji wa kesi zote unasitishwa kwa muda wa siku 30 kuanzia tarehe 26 Machi, 2020 hadi tarehe 24, April, 2020. Kwa zile kesi ambazo ziko katika hatua ya 'submission', Mahkama husika itawashauri Mawakili au wenye kesi kuwasilisha kwa maandishi.

2. Mahkama zitashughulikia kesi za dharura na kwa washtakiwa wenye kesi nzito na maombi ya dhamana. Muombaji na wakili wake au kwa ombi la dhamana wadhamini ndio watakaoruhusiwa kuingia Mahkamani.

3. Kwa makosa yenye dhamana, Majaji na Mahakimu wanatakiwa kutoa dhamana yenye masharti nafuu iii kupunguza mrundikano katika Chuo cha Mafunzo kwa kipindi hichi.

4. Katika kipindi hichi, watendaji wote wa Mahkama wataendelea kuwepo kazini. Hata hivyo, Kumbi za Mahkama (Open Court) hazitatumika. Kwa

Majaji na Mahakimu wenye Hukumu na Maamuzi (Ruling) watatumia kipindi hichi katika kuzikamilisha.

5. Zaidi ya muongozo uliotolewa hapo juu 'sanitizers'. na hatua nyengine za kinga zinawekwa.

Muongozo huu unaweza kurekebis hwa wakati wowote kufuatana na maelekezo yatakayotolewa na Serikali.

Huduma za Tehama

Barua Pepe Msaada wa kisheria

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

MAHAKAMA DPP WAKFU LRC SADC IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 772, Mazizini, Zanzibar
Tel.: +255(24)2234683 Mhe WaziriTel.: +255 (24)2234684 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2234689
Email: info@sheriasmz.go.tz