Head image
Govt. Logo

Hits 40090 |  1 online

     
Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mhe, Khamis Juma Mwalim amezindua Jarida la Tume ya kurekebisha sheria.
news phpto

Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mhe, Khamis Juma Mwalim amezindua Jarida la Tume ya kurekebisha sheria ili kufikisha elimu sahihi ya sheria kwa wananchi.

Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mhe, Khamis Juma Mwalim amezindua Jarida la Tume ya kurekebisha sheria ili kufikisha elimu sahihi ya sheria kwa wananchi.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe, Khamis amesema wananchi wengi wanapojua sheria wanajitahidi kuepuka makosa mbali mbali ya uvunjifu wa sheria hivyo amewataka watendaji kuhakikisha Jarida hilo linawafikia wananchi hasa wa vijijini ili lengo la tume hiyo liweze kufikiwa.

Amesema Jarida hilo likiwafikia wananchi litawasaidia kupata uelewa wa sheria mbali mbali ambazo zipo nchini na kuweza kuishi kwa amani na upendo katika jamii.

Aidha, amewataka kuendelea kushirikiana katika kufanyia marekebisho sheria zilizopitwa na wakati ili kwenda sambamba na mahitaji kwa wakati husika.

Mhe, Khamis ameipongeza Tume hiyo kwa mashirikiano mazuri na wizara jambo ambalo limeweza kusaidia kupatikana kwa mafanikio makubwa.

Mwenyekiti wa tume hiyo Mhe, Jaji Mshibe Ali Bakari amewataka watendaji hao kujiendeleza zaidi kielimu kwani hatua hiyo itawasaidia kuaminika zaidi katika kazi zao na kuwa tofauti na wengine.

Aidha, amewataka waandishi wa Jarida hilo kuzingatia zaidi maadili, kanuni za uandishi, lugha sanifu na lugha za kisheria ili kuleta uelewa mpana kwa watu.

Naye, Katibu wa Tume hiyo Ndg, Kubingwa Mashaka Simba amesema Jarida hilo limekusudia kukuza uelewa kwa wananchi katika masuala ya sheria za nchi.

Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya watendaji wa Jarida hilo Ndg, Nassor Ameir Tajo ameahidi kuendeleza ushirikiano na kuendelea kufanya kazi kwa bidii na uzalendo ili kuhakikisha malengo ya serikali kwa tume hiyo yanaweza kufikiw

Huduma za Tehama

Barua Pepe Msaada wa kisheria

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

MAHAKAMA DPP WAKFU LRC SADC IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 772, Mazizini, Zanzibar
Tel.: +255(24)2234683 Mhe Waziri



Tel.: +255 (24)2234684 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2234689
Email: info@sheriasmz.go.tz