Head image
Govt. Logo

Hits 70215 |  6 online

     
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Haasan Mwinyi akiapa kuongoza Zanzibar kwa awamu ya 8 kuanzia 2020-2025.
news phpto

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Haasan Mwinyi akiapa kuongoza Zanzibar kwa awamu ya 8 kuanzia 2020-2025.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amewapongeza Wazanzibari kote nchini kwa kujitokeza kwa wingi na kutumia vyema haki yao ya kikatiba ya kushiriki katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Dk. Mwinyi ametowa pongezi hizo leo katika sherehe za kuapishwa kuwa Rais wa Awamu ya nane ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, hafla iliyofanyika katika Uwanja wa Amani Jijiji hapa.

Amesema hatua ya wananchi hao kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi huo na hatimae kukichaguwa Chama cha Mapinduzi ni kielelezo cha kukomaa kisisasa na kidemokrasia, kwa kutambua kuwa uchaguzi ulio huru na haki ndio njia sahihi ya kupata viongozi wataongoza Serikali kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Alisema hatua hiyo ni kielelezo cha kuthibitisha upendo kwa chama cha Mapinduzi, hivyo akaahidi kuwatumikia wananchi wote ili kuinua hali zao.

Aidha, Dk. Mwinyi aliwapongeza wananchi na wanachama wa CCM kwa kusherehekea ushindi mkubwa uliopata chama hicho kwa amani na utulivu kwa kuelewa kuwa jamo hilo kubwa na muhimu sana na msingi wa maendeleo ya Taifa.

Aliwapongeza wagombea Urais kupitia vyama mbali mbali vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi huo kwa kukubali matokeo yaliotangazwa na Tume ya Chagzui Zanzibar (ZEC) na hivyo akaahidi kushirikiana nao katika kuijenga Zanzibar.

Rais Dk. Mwinyi alieleza kuwa kauli na ahadi za viongozi hao zilizowasilishwa na Mgombea wa Urais kupitia Chama cha ADA TADEA, Juma Ali Khatib zimempa matumaini makubwa katika kufanikisha azma yake ya kuijenga Zanzibar mpya, akiahidi kushirikiana na viongozi hao katika kuwaletea maendeleo wananchi wote bila ubaguzi wa aina yoyote, sambamba na kuahidi kuongoza kwa kuzingatia Katiba ya Zanzibar.

Alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, awamu ya saba Dk. Ali Mohamed Shein klwa kumpa muongozo na ushirikiano katika hatua zote za kmapeni hadi kukiwezesha chama hicho kupata ushindi mkiubwa.

Vile vile aliipongeza Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kwa kutimiza vyema majukumu yake ya Kikatiba ya 1984 Ibara ya 119 na 120 na sheria ya klaunzisha Tume hiyo kwa kuandaa na kusimamia uchaguzi na hatimae kutangaza matokeo Oktoba 29, 2020.

Dk. Mwinyi alisema serikali atakayoiunda itaongozwa kwa misingi ya haki, uwajibikaji, uwazi na usawa kwa wananchi wote bila kumbagua mtu kutokana na itikadi yake, jinsia au eneo analotoka.

Aliwashukuru Mabalozi na wawakilishi wa mashirika mbali mbali ya kimataifa walioshiriki katika sherehe hizo na kubainisha kuwepo kwao kunathibitisha uhusiano mwema uliopo kati ya Zanzibar na nchi zao.

Mapema, Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee alimkaribisha Rais wa Zanzibar , akibainisha hamu waliyonayo wnanachi ya kumsikiliza.

Huduma za Tehama

Barua Pepe Msaada wa kisheria

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

MAHAKAMA DPP WAKFU LRC SADC IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 772, Mazizini, Zanzibar
Tel.: +255(24)2234683 Mhe WaziriTel.: +255 (24)2234684 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2234689
Email: info@sheriasmz.go.tz