Hits 30030 | 2 online
Dkt Mwinyi Talib Haji ateuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu Zanzibar.
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu Namba 55(1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemteua Dkt. Mwinyi Talib Haji kuwa MWANASHERIA MKUU WA ZANZIBAR.
Kabla ya Uteuzi huo Dkt. Mwinyi Talib Haji alikuwa Naibu Katibu Mkuu Katika Wizara ya mambo za nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Uteuzi huo umeanzia leo tarehe 03 Novemba, 2020.