Head image
Govt. Logo

Hits 27736 |  1 online

     
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Mhe Haroun Ali Suleiman amewataka wakuu na watendaji wa taasisi ya Ofisi hio kuzidisha mashirikiano ya kiutendaji
news phpto

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Mhe Haroun Ali Suleiman amewataka wakuu na watendaji wa taasisi ya Ofisi hio kuzidisha mashirikiano ya kiutendaji na kuwa wawazi kwa maamuzi wanayoyatoa

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Mhe Haroun Ali Suleiman amewataka wakuu na watendaji wa taasisi ya Ofisi hio kuzidisha mashirikiano ya kiutendaji na kuwa wawazi kwa maamuzi wanayoyatoa kwa kutambua dhamira ya Serikali ya awamu ya nane ya kufanyakazi kwa bidii.

Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano ya Ofisi na aliyekuwa waziri wa Katiba na Sheria awamu ya saba Mhe Khamis Juma Mwalim, Mhe Haroun amesema kila mtendaji anapaswa kufahamu majukumu na dhamana zake bila kusukumana pamoja kuhakikisha taarifa na maamuzi yoyote yayotolewa yawe yanamfikia na waziri husika .

Nae Waziri mstaafu wa Katiba na Sheria Mhe Khamis Juma Maalim amewashukuru watendaji wote katika kipindi chote cha uongozi wake na kuwataka kuendeleza mshikamano katika majukumu yao ya kazi

Aidha Ndugu Mwalim amemkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Mhe Haroun Ali Suleiman zana za kufanyia kazi ikiwemo hotuba ya bajeti 2020-2021, sheria mbali mbali zinazoongoza utendaji wa taasisi za sekta ya sheria, pamoja na mpango kazi na kuelezea baadhi ya changamoto zilizobakia ambazo hazikutekelezeka katika awamu ya 7 .

Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na kuimarisha uendeshaji wa kesi mahakamani na kuwezesha uendeshaji wa kesi kwa njia ya kielektroniki, Kutomalizika kwa ujenzi wa Mahakama kuu, kuanza kufanya kazi kwa mfuko wa Hijja na kuanza rasmi kwa skuli za sheria Zanzibar,

Huduma za Tehama

Barua Pepe Msaada wa kisheria

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

MAHAKAMA DPP WAKFU LRC SADC IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 772, Mazizini, Zanzibar
Tel.: +255(24)2234683 Mhe Waziri



Tel.: +255 (24)2234684 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2234689
Email: info@sheriasmz.go.tz