Hits 86458 | 3 online
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria na Ndg George Joseph Kazi amesema Jumuiya ya Mawakili itakayoanzishwa itakuwa ni ya kitalaamu itakayoendeshwa na wataalaam wenye sifa zinazohitajika kulingana na fani yao ya sheria.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria na Ndg George Joseph Kazi amesema Jumuiya ya Mawakili itakayoanzishwa itakuwa ni ya kitalaamu itakayoendeshwa na wataalaam wenye sifa zinazohitajika kulingana na fani yao ya sheria
George Kazi ameyasema hayo alipokuwa akielezea mapendekezo juu ya umuhimu wa kuanzishwa kwa Jumuiya ya Mawakili Zanzibar kwenye semina ya uelewa kwa Kamati ya Sheria, Utawala Bora na Idara Maalum za SMZ kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika ukumbi wa Ofisi za Serikali Gombani Chakechake Pemba
Ndugu George amesema kukosekana kwa sheria zisizo rasmi zinazosimamia kazi za Mawakili kumesababisha matatizo mengi ikiwemo kukosekana uwakilishi mzuri wenye weledi kwa wananchi wanaohitaji kusaidiwa kwenye vyombo vya sheria na ushauri wa kisheria , kukosekana kwa usimamizi mzuri wa ukusanyaji wa mapato .
Kutokana na chagamoto hizo Wizara ya Katiba na Sheria imeona ipo haja ya kuwa na Jumuiya ya Mawakili itakayoanzishwa kisheria, sheria inayokidhi haja ya matakwa ya wazanzibari kwa kuzingatia mazingira na kutatua chanagamoto zinazojitokeza katika usimamizi wa Jumuiya ya Mawakili