Head image
Govt. Logo

Hits 70200 |  7 online

     
Wananchi msisite kutoa maoni na ushauri
news phpto

Mashirikiano ya pamoja kutoka kwa wanufaika wa huduma ya msaada wa kisheria na watoaji huduma hio ndio chachu itakayopelekea utekelezaji mzuri wa majukumu ya Idara ya Msaada wa Kisheria katika kuleta ufanisi wa majukumu ya kazi.

Mashirikiano ya pamoja kutoka kwa wanufaika wa huduma ya msaada wa kisheria na watoaji huduma hio ndio chachu itakayopelekea utekelezaji mzuri wa majukumu ya Idara ya Msaada wa Kisheria katika kuleta ufanisi wa majukumu ya kazi

Mkurugenzi wa Idara ya Msaada wa Kisheria Bi Hanifa Ramadhan Said ameyasema hayo kwenye mkutano uliowashirikisha baadhi ya wanufaika wa msaada wa kisheria uliofanyika katika ukumbi wa mkutano Wizara ya Katiba na Sheria Mazizini

Bi Hanifa amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeanzisha Idara ya Msaada wa Kisheria ili kuratibu utoaji na upatikanaji wa huduma ya kisheria kwa wananchi wote bila ya kujali uwezo wa kifedha kwa mtaka huduma

Aidha Bi Hanifa amewashukuru wanufaika hao waliopatiwa msaada kutoka vituo vinavyotoa huduma za msaada wa kisheria kwa kukubali kufuata taratibu na kutoa mashirikiano pale wanaposhughulikiwa malalamiko yao jambo ambalo linarahisisha kupata haki zao stahiki kwa muda muafaka

Pia ametoa pongezi za dhati kwa watoaji wa huduma ya msaada wa Kisheria kwa kuwapokea na kuwashughulikia matatizo yao wananchi bila upendeleo jambo ambalo limepelekea kutokuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wanufaika waliofika katika vituo vyao

“nimefarijika na michango iliyotolewa leo hii kutoka kwenu hakuna hata mmoja aliyelalamika kuwa hakutendewa haki wakati alipotaka huduma ya msaada wa Kisheria na mmeona mafanikio yake hivyo msisite kuwafahamisha na wengine pale wanapopata matatizo hasa wanapodai haki zao za msingi wasiyamalize kienyeji au kuona muhali bali wafuate taratibu, vituo hivi vipo kwa ajili yenu”alisisitiza

Hata hivyo amewaomba kutosita kutoa maoni ama ushauri kwa Idara ya Msaada wa Kisheria ili kuenda sambamba na kasi ya maendeleo kwani lengo la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni kukuza ustawi wa wananchi wake katika nyanja zote za maisha kwa kuwahudumia na kuwaletea maendeleo na kuwaondolea uzito wa maisha wananchi wake

Bi Hanifa ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuweza kufanikisha kupatikana sera, sheria na kanuni inayosimamia sekta nzima ya msaada wa kisheria

Wakitoa mada kuhusu huduma za msaada wa kisheria watoa mada katika mafunzo hayo wanasheria ndugu Amour Omar Mbwana na Omar Haji Gora wamesema huduma za msaada wa Kisheria zinajumuisha ushauri wa kisheria, uwakilishi mahakamani au katika mabaraza, kutoa elimu ya kisheria, pamoja na kutayarisha nyaraka za kisheria na taarifa kuhusiana na mambo ya kisheria

Aidha wamefafanua baadhi ya vifungu kwa watu wasiokuwa na sifa ya kupatiwa msaada wa kisheria kuwa ni pamoja na kampuni, shirika, taasisi ya umma, Jumuiya ya kiraia , Jumuiya isiyokuwa ya kiserikali au mtu mwengine wa kisheria .

Msisitizo pia umewekwa kuwa watoaji wa msaada wa kisheria hawatatoa huduma za msaada wa kisheria kuhusiana na kesi za madai zikiwemo masuala yanayohusu ulipaji wa kodi, ulipaji wa madeni na katika kesi za ufilisi na kutoweza kulipa madeni

Nao washiriki wa mafunzo hayo wametoa shukurani zao kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuanzisha Idara ya Msaada wa Kisheria na kuiomba idara hio kuendelea kutoa elimu na kuielimisha jamii ili waweze kuifahamu na kuona umuhimu wa kufikisha malalamiko yao pale wanapohitaji usaidizi wa huduma ya msaada wa kisheria

Washiriki hao wamezungumzia kuwa utaratibu huo wa kuwasaidia kisheria wananchi wasiokuwa na uwezo ni jambo jema , na kusema kuwa Serikali inastahili kupongezwa kwa sababu wamo wananchi wengi wanyonge wenye vilio vya muda mrefu, lakini hawana pa kuvipeleka kutokana na unyonge.

Wameeleza kuwa jambao la muhimu kwa Taasisi inayohusika na Utoaji wa Huduma za msaada wa Kisheria kuhakikisha wasiokuwa na uwezo ndio wanaonufaika na utaratibu huo na kuomba kufanywa kila liwezekanalo kuwazuia wale wenye uwezo wa kujisimamia na kuendesha kesi na kupata haki zao wenyewe kutojingia katika utaratibu huo na kuwazuia walengwa.

Wamesema kwamba wamo wananchi wengi ambao uwezo wao na mwamamko wa kupigania haki zao ni mdogo, huku baadhi ya wananchi hao wanashindwa na hata nauli ya kuwawezesha kufika mahakamani, hivyo uamuzi huo ni jambo la kupongezwa kwa sababu umelenga hasa kuwakomboa wenye mahitaji.

Huduma za Tehama

Barua Pepe Msaada wa kisheria

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

MAHAKAMA DPP WAKFU LRC SADC IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 772, Mazizini, Zanzibar
Tel.: +255(24)2234683 Mhe Waziri



Tel.: +255 (24)2234684 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2234689
Email: info@sheriasmz.go.tz