Hits 56923 | 2 online
RAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN AFUNGUA MKUTANO WA JUMUIYA YA MAHAKIMU NA MAJAJI ZANZIBAR.
Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein Amesema Matumizi mazuri ya ardhi na usimamizi bora wa mazingira ni misingi muhimu katika maendeleo ya nchi yoyote duniani.
Akizungumza katika Mkutano wa mwaka wa jumuiya ya Majaji na Mahakimu wa nchi za Afrika Mashariki unaofanyika hoteli ya Madinatil Al Bahri, Dk Shein amesema kuongezeka kwa idadi ya watu na kukua kwa uchumi kumeleta matatizo mengi katika sekta ya ardhi na mazingira hali inayorudisha nyuma maendeleo ya nchi hizo.
Hivyo amesema iwapo hali hiyo itaendelea itakua ni tishio kwa maendeleo ya kiuchumi na usalama kwa nchi za Afrika Mashariki.
Aidha amesema katika kutatuwa matatizo hayo wakati umefika kwa kwa nchi nyingi za afrika Mashariki kuweka mikakati ya kuimarisha Mazingira na Matumizi mazuri ya Ardhi, na kueleza matumaini yake kua Mkutano huo utaweka njia mbadala za kutatua matatizo yaliyopo.
Pia Dk Shein aliitaka jumuiya hiyo kushirikiana na taasisi mbali mbali za Serikali katika masuala ya kimazingira hasa ikizingatiwa kwamba uchumi wa nchi za Afrika Mashariki Tunaendelea kukua katika sekta ya Mafuta na Gesi.
Nae Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh. Omar Othman Makungu amepongeza juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuwapatia mazingira mazuri
Mkutano huo wa siku nne unahudhuriwa na Majaji na Mahakimu zaidi ya 350 kutoka nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Sudani ya Kusini, Tanzania Bara, Kenya, Ruwanda, Burundi pamoja na wenyeji Zanzibar.