Hits 38519 | 2 online
Mkurugenzi Wa Idara ya Msaada wa Kisheria Bi Hanifa Ramadhan Said wa Mwanzo kushoto akiongoza kikao kilichojadilin mwelekeo wa kukusanya taarifa ya robo mwaka cha kuratibu masuala ya Msaada wa Kisheria.
Imeelezwa kuwa ili kupata tathmini halisi ya utekelezaji wa masuala ya msaada wa kisheria ni jukumu la watoaji msaada wa kisheria pamoja na wadau kuweka vizuri taarifa za watu wanaowapa huduma za msaada wa kisheria
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Idara ya Msaada wa Kisheria Bi Hanifa Ramadhan Said wakati alipokutana na washirika na watoaji wa msaada wa kisheria kutoka taasisi za Serikali na taasisi binafsi ili kuweka mikakati na mipango imara juu ya mwelekeo na namna ya kuwasilisha ripoti ya robo mwaka
Bi Hanifa amesema Utekelezaji mzuri wa vikao vya robo mwaka ndio utakaoleta ufanisi wa utendaji kazi ambao utarahisisha huduma za msaada wa kisheria na kuiwezesha Serikali kupata taarifa za uhakika na zilizosahihi na zilizosahihi juu ya masuala ya huduma za msaada wa kisheria.
“ watoaji wa huduma za msaada wa kisheria ni watu muhimu sana na ndio maana kila hatuwa tuko nanyi kupanga mambo mbali mbali yanayohusu huduma za msaada wa Kisheria naomba mashirikiano yenu toweni michango juu ya mwelekeo wa uwasilishaji taarifa ili tutakapotaka taarifa na ripoti za kila robo mwaka za watoaji wa huduma za msaada wa kisheria msisite kutuwasilishia kwa wakati wananchi wanatutegemea na Serikali imetuamini”.
Aidha Bi Hanifa amesema jukumu la watoaji msaada wa kisheria ni kuweka vizuri taarifa za watu wanaowapa huduma za msaada wa kisheria, taarifa ambazo zinatakiwa ziambatanishwe na aina ya huduma zilizotolewa ikiwemo Ushauri, msaada, uwakilishi au elimu
Wakitoa michango yao baadhi ya washiriki wa kikao wameomba mashirikiano zaidi ikiwa ni pamoja na kuongeza nguvu Wilayani na kuwashirikisha wadau wote , kuweka mfumo wa aina moja wa uwasilishaji wa ripoti hizo, kuendelea kutoa elimu ili jamii iweze kufahamu majukumu ya Idara hiyo
Pia wameitaka Idara ya Msaada wa Kisheria kuwafikia watu wenye mahitaji maalum wakiwemo watu wenye ulemavu kulingana na mahitaji yao pamoja kuwafikia wanafunzi katika skuli mbalimbali mjini na vijijini
Miongoni mwa kazi za Idara ya Msaada wa Kisheria ni Kupokea na kujumuisha ripoti za robo mwaka kuhusiana na huduma za msaada wa kisheria na mambo mengine kwa ajili ya kuwasilishwa mbele ya Katibu Mkuu pia kupokea na kujumuisha taarifa za mwaka za watoaji wa msaada wa kisheria.
Nae Afisa Sheria kutoka Idara ya Msaada wa Kisheria ndg Ali Haji Hassan amewaomba Watoa huduma za msaada wa kisheria kuongeza juhudi katika kuwajengea uwezo wananchi, kufahamu haki zao za msingi na wanapata huduma ipasavyo.
Baadhi ya taasisi zilizoshiriki ni pamoja na wawakilishi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, Jeshi la polisi, ustawi wa jamii, Idara ya watu wenye ulemavu, chuo cha mafunzo,Tawala za Mikoa, Kituo cha hudumaza sheria Zanzibar – ZLSC.
Jumuiya ya wanasheria wanawake Zanzibar ZAFELA, Chama cha waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar -TAMWA, Jumuiya ya mawakili Zanzibar ZLS, Mtandao wa wasaidizi wa Sheria Zanzibar -ZAPANET, Umoja wa Watu wenye Ulemavu Zanzibar, PIRO na LSF
Idara ya Msaada wa Kisheria Zanzibar ni taasisi iliyo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria yenye dhamana ya kuratibu, kuendesha na kusimamia utoaji wa msaada wa kisheria.
Huduma za msaada wa kisheria hutolewa na watoaji huduma hizo ambao ni Mawakili, Wanasheria, Mavakili au Wasaidizi wa Sheria pamoja na Taasisi au Jumuiya zilizosajiliwa kwa lengo la kutoa msaada wa kisheria.