Hits 70214 | 6 online
Katibu Mkuu Wizara Katiba na Sheria ndg George Kazi akiwa na Mkurugenzi Mipango Sera na Utafiti Bi Daima Mkalimoto
Wizara ya Katiba na Sheria imesema mabadiliko ya sekta ya sheria yanayofanywa na seriklai ni kwa ajili ya kukuza uwezo wa watendaji wa taasisi za wizara hiyo pamoja na kuwa mifumo bora ya utoajihaki kwa wananchi
Katibu Mkuu Wizara hiyo George Kazi ameyasema katika kikao cha wakuu wa taasisi za Wizara hiyo ili kupata maoni ya mpango wa kuimarisha sekta ya sheria Zanzibar
Amesema sekta hiyo inahitaji kuimarishwa ili kuenda saambamba na mabadiliko ya teknolojia pamoja na kufikia dira ya maendeleo ya Zanzibar katika sekta ya sheria
Wakitoa michango yao wataalamu hao wameomba kuzingatiwa utoaji na upatikanaji wa haki, kujali makundi maalum, jinsia , uendeshaji wa shughuli ya sekta ya sheria, uwazi , uadilifu na uwajibikaji
mshauri muelekezi katika masuala ya sekta ya Umma Lufumbi amewataka wataalamu hao kutoa ushirikiano ili mkakati wa kuimarisha sekta ya umma unaoandaliwa kuwa na maslahi mazuri kwa maendeleo ya Wizara ya Katiba na ya Taifa
Kikao hicho kimeamdaliwa Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Shirika la maendeleo la kimataifa UNDP