Head image
Govt. Logo

Hits 70160 |  3 online

     
Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mhe Khamis Juma Mwalim akisoma hotuba kwenye mkutano wa Majaji Wakuu wa dunia kuhusu haki za watoto duniani uliofanyika Lucknow India.
news phpto

Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mhe Khamis Juma Mwalim akisoma hotuba kwenye mkutano wa Majaji Wakuu wa dunia kuhusu haki za watoto duniani uliofanyika Lucknow India.

Kwa miaka kadhaa Serikali za duniani kote zimekuwa zikipigania haki za watoto na haki za binaadamu pamoja na kuweka vipaumbele muhimu ambapo taasisi za kijamii na za kimataifa zimekuwa zikiainisha mahitaji ya makundi maalum katika jamii zinazohitaji huduma muhimu na za kipekee ili kulinda ustawi wa watoto

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Khamis Juma Mwalim ameeleza hayo wakati akiwasilisha mada kuhusiana na haki za watoto kwenye mkutano Mkuu wa 20 wa Majaji wa Dunia unaofanyika katika ukumbi wa Lucknow nchini India.

Amesema makundi ya Watoto yanakabiliwa na matukio tofauti ya ukatili, kushindwa kupata haki zao kutokana na kudhulumiwa kiakili, kiwiliwili na kimaadili pamoja na kukosa kupata mahitaji yao ya msingi.

Ameeleza kuwa matatizo hayo yanachangiwa kwa kukosekana ufahamu dhidi ya ulinzi wa haki ya watoto, muhali, aibu na vikwazo katika familia zenye migogoro kwa misingi ya Imani na kukosa msaada wa uchumi wa familia.

Waziri khamis amefahamisha kuwa kuna haja ya kuanzisha utaratibu maalum wa kupambana na unyanyasaji wa aina zote dhidi ya watoto kupitia sheria ya kimataifa inayolinda watoto itakayotekelezwa duniani kote.

“Ukatili dhidi ya watoto uko kila mahali duniani ndio maana sababu dunia inapaswa kuungana pamoja katika kupigania na kulinda ustawi wao na kuunda sheria na mifumo madhubuti ya kukabiliana na ukiukwaji wa haki za watoto.”

Ameongeza kuwa ana Imani kuwa Mkutano huu, umedhamiria kushawishi dunia kuwafanya watoto kuwa huru dhidi ya ubaguzi wa wanaotendewa pamoja na kuwanusuru na majanga yanayotokana na vurugu.

Bunge moja la dunia linahitajika kwa lengo la kulinda watoto,vizazi vijavyo na jamii kwa ujumla dhidi ya vita vinavyoendelea katika nchi mbalimbali pamoja na matishio ya ugaidi.

Amesema Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Tanzania imeridhia mikataba mbali mbali na matamko kadhaa ya kimataifa ya kulinda haki za mtoto

Kutokana na mikataba hio Zanzibar imeweka sera mbali mbali na sheria zinazoendana na mikataba hiyo na kutolea mfano sheria ya mtoto ya mwaka 2011, Sheria ya elimu ya mwaka 1982 na sheria ya adhabu ya mwaka 2018 ambazo kwa pamoja amesema zimeelezea haki zote za msingi za mtoto na ulinzi wake .

Akiifafanua haki ya kupata elimu Waziri Khamis amesema imepewa umuhimu wa kipekee na ndio maana sera ya elimu na afya ya Zanzibar zinaeleza kuwa elimu bila malipo na matibabau ya Afya bure kwa kila mtoto na wananchi kwa ujumla

Aidha ameilezea sheria ya kazi ya mwaka 2005 inayomlinda mtoto na ajira za utotoni pamoja na kuelezea namna Zanzibar inavyochukulia suala la mtoto kwa umakini mkubwa na ndio maana imewekewa Wizara maalum

Aidha Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi ya mwaka 2005 kwa pamoja sheria hizi mbili zinakataza aina mbaya zaidi ya ajira kwa watoto na inakataza mtoto chini ya umri wa miaka 18 kuajiriwa kwenye mgodi, kiwanda au kama wafanyakazi kwenye meli au mtu mwingine yeyote, ambapo hali za kazi zinaweza kuzingatiwa kuwa hatari.

Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Wazee, Wanawake na Watoto inasimamia haki za watoto, inashughulikia changamoto zinazowakabili vijana na watoto, kukuza mazingira mazuri ya utunzaji bora na ustawi wa watoto na pia kutunza watoto yatima.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefanya jitihada za makusudi katika kukuza haki za watoto kwa kuanzisha dawati maalum linaloitwa jinsia na watoto kwa wahanga wa unyanyasaji wa watoto na unyanyasaji wa kijinsia ambayo yapo katika vituo vya polisi

Hivi karibuni , Baraza la Mwakilishi wa Zanzibar limetunga Sheria ya Msaada wa Sheria Namba 13 ya 2018 ambayo hutoa kwa urahisi ulinzi wa haki za watoto kupitia huduma za bure za Msaada wa Kisheria.

Katika kufanikisha azma ya Mkutano huo amesema ulimwengu unahitaji kuwa huru usio na ubaguzi dhidi ya watoto na uhuru kutokana na janga la vita, hivyo kuna haja ya kuanzisha utaratibu maalum wa kupambana na unyanyasaji wa aina zote dhidi ya watoto kupitia sheria ya ulimwengu inayotekelezwa kwa watoto ambayo inaweza kutekelezwa kila mahali kote ulimwenguni.

Waziri Khamis amewasilisha mada inayozungumzia kuunganisha ulimwengu kwa watoto kupitia sheria zinazotekelezeka za ulimwengu na utawala bora na amemalizia kwa kusisitiza kuimarishwa kwa Amani, ulinzi na usalama na maendeleo endelevu kwa ajili vizazi vijavyo

Katika mkutano huo Zanzibar inawakilishwa na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Khamis Juma Mwalimu akiwa ameongozana na Jaji Mkuu Mhe Omar Othman Makungu, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ndg Kai Bashiru na Mrajis wa Mahakama Kuu Zanzibar ndg Mohamed Ali Shein.

Huduma za Tehama

Barua Pepe Msaada wa kisheria

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

MAHAKAMA DPP WAKFU LRC SADC IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 772, Mazizini, Zanzibar
Tel.: +255(24)2234683 Mhe WaziriTel.: +255 (24)2234684 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2234689
Email: info@sheriasmz.go.tz