Hits 38524 | 1 online
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Zanzibar Ndg George Joseph Kazi ameongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Afrika Kusini Johannesburg kuhudhuria Mkutano wa Wataalamu wa Sheria wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Zanzibar Ndg George Joseph Kazi ameongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Afrika Kusini Johannesburg kuhudhuria Mkutano wa Wataalamu wa Sheria wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC
Mkutano wa Wataalamu wa Sheria wa SADC ulioanza tarehe 9 hadi tarehe 13 Disemba 2019 ni utekelezaji wa maamuzi ya mkutano wa Kamati ya Wanasheria Wakuu, Mawaziri wa Katiba na Sheria wa SADC uliofanyika Julai 2018
Pamoja na mambo mengine nchi wanachama zilielekezwa kuhuisha Sheria za nchi zao zinazohusisha urejeshaji wa wahalifu katika nchi wanazotuhumiwa kufanya uhalifu na ushirikiano wa masuala ya kisheria katika makosa ya jinai
Mkutano huo ulipokea na kujadili maoni na mapendekezo yatokanayo na masuali yaliyowasilishwa kwa nchi wanachama katika kuwezesha utekelezaji wa itifaki ya Jumuiya ya Ushirikiano wa masuala ya kisheria katika makosa ya Jinai na itifaki ya urejeshaji wa wahalifu katika nchi wanazotuhumiwa kufanya uhalifu
Aidha mkutano pia ulitoa wasilisho rasmi la namna sheria zao za nchi zinavyotekeleza masuala ya urejeshaji wa wahalifu katika nchi wanazotuhumiwa kufanya uhalifu kwa kuainisha taratibu, wadau muhimu wanaohusika, muda wa utekelezaji wa masuala hayo na changamoto zilizopo ndani ya nchi zao katika utekelezajiwa sheria hizo
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndio Mwenyekiti wa sasa wa SADC hivyo Mkutano huo umeongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Tanzania Profesa Sifuni Mchome
Wajumbe wengine waliohudhuria mkutano huo kutoka Tanzania ni Naibu Mwanasheria Mkuu Dkt Evaristo E. Longopa, Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Katiba na Sheria Tanzania Bara Bi Mercy Mrutu, Wakili wa Serikali Mwandamizi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Felista S. Lelo, Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi Zulekha Fundi.