Hits 86476 | 2 online
Maafisa wa Habari na Tehama wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Ndg George J. Kazi, Mkurugenzi wa Idara ya Msaada wa Kisheria Bi Hanifa Ramadhan Said pamoja na Wawezeshaji wa mafunzo hayo.
Katibu mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria ndg. George J. Kazi amewataka maafisa Habari na Mawasiliano Maafisa Tehama wa taasisi za Wizara hiyo kufanya kazi kwa mashirikiano na kutoa habari kwa wakati ili wananchi wapate kujua mambo yanayofanywa na Wizara na taasisi zake.
Akifungua mafunzo kwa maafisa hao amesema Wizara inafanya kazi nyingi ambazo wananchi wanahaki ya kuzijua ikiwemo kusimamia na kuendeleza utekelezaji wa sera na mipango katika masuala ya sheria na katiba, usimamizi wa upatikanaji haki, ushauri wa kisheria na utayarishaji wa misaada ya sheria.
Katibu George amewataka maafisa hao kufahamu vyema Taasisi zao na vitendea kazi muhimu ili hata wanapotoa taarifa wafahamu kiundani kama ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi
“Maafisa habari na maafisa wa teknolojia (ICT) Maafisa habari mnatakiwa kuwa wabunifu na kuwa watendaji mnaojituma katika kuonesha mafanikio ya utekelezaji kwa kutetea na kutoa ushauri lakini pia kuwa kiungo kati ya Wizara na jamii inayotuzunguka”.
Muezeshaji katika mafunzo hayo Ali Sultan amewashauri maafisa habari na mawasiliano kuvitumia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwani ina nguvu kubwa ya kufikisha ujumbe kwa jamii kwa haraka zaidi.
Ndg Ali amewataka maafisa hao kutumia ujuzi wao na kuhakikisha wanatoa taarifa sahihi zinazohusu wizara kupitia tovuti yao ya Wizara, televisheni, redio, magazeti, majarida, mitandao ya kijamii ili wananchi kufahamu majukumu ya Wizara
Washiriki wa mafunzo hayo wameahidi kuifanyia kazi kwa vitendo elimu waliyoipata na kufanya kazi kwa kushirikiana kwa lengo la kurahisisha utendaji wao wa kazi.
Aidha wamesema mafunzo hayo pia yatawasaidia kupanga mikakati ya pamoja na kuimarisha mawasiliano pamoja kutoa ushauri mzuri kulingana na nafasi zao za kazi
Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi wa Wizara Juma Ali Simai akifunga mafunzo hayo amesema maafisa wa habari na mawasiliano ni daraja kati ya watendaji wa taasisi za Serikali na jamii hivyo ni vyema kutekeleza majukumu yao ya kuripoti utekelezaji wa mipango kazi ya Serikali kwa wananchi.
Jumla ya mada 5 zimewasilishwa katika mafunzo hayo yakiwemo Umuhimu wa Afisa Habari, kazi na majukumu ya Afisa Habari, Uandaaji wa Documentari, Kuhariri video na uandishi wa skript, Jinsi ya kuandaa Press Release, namna ya kuandaa Press Comference
Lengo la mafunzo hayo ni kuwamarisha kiutendaji, kufahamu na kuwakumbusha majukumu ya kazi, kuwa na mkakati wa pamoja na kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi katika masuala yanayohusu Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na Taasisi zake.