Hits 70217 | 6 online
RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMMED SHEIN AMESEMA KUIMARISHWA KWA MIUNDOMBINU YA SEKTA YA SHERIA KUNAASHIRIA KUWEPO KWA UTAWALA BORA KATIKA NCHI.
MKOA WA KUSINI UNGUJA
RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMMED SHEIN AMESEMA KUIMARISHWA KWA MIUNDOMBINU YA SEKTA YA SHERIA KUNAASHIRIA KUWEPO KWA UTAWALA BORA KATIKA NCHI.
AKIWEKA JIWE LA MSINGI LA JENGO LA MAHAKAMA KUU HUKO TUNGUU IKIWA NI MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA, AMESEMA UJENZI HUO NI UTEKELEZAJI WA MPANGO WA SERIKALI KATIKA KUIMARISHA SEKTA YA SHERIA KAMA ILIVYO KATIKA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI.
AMESEMA ONGEZEKO LA WATU NCHINI NI VYEMA LIKAENDANA NA UPATIKANAJI WA MAENDELEO KATIKA SEKTA ZOTE ZA KIJAMII IKIWEMO UPATIKANAJI WA HAKI ZAO.
AIDHA DR SHEIN AMESISITIZA KWA WATUMISHI WA UMMA KUFANYAKAZI KWA UADILIFU NA AKAWAONYA WATENDAJI WANAOHUSIKA NA MANUNUZI KUACHA TABIA YA UBABAISHAJI KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAO ILI KUEPUKA KUITIA HASARA SERIKALI.
NAE JAJI MKUU WA ZANZIBAR MHE, OMAR OTHMAN MAKUNGU AMEMSHUKURA RAIS WA ZANZIBAR KWA JUHUDI ZAKE ZA KUIMARISHA MAHAMAMA NCHINI KWA KUONGEZA BAJETI YA MAHAKAMA.
UJENZI WA MAHAKAMA KUU UNAOENDESHWA NA KAMPUNI YA ADVENT YA DAR ES SALAAM, UTAGHARIMU ZAIDI YA SHILINGI BILION 14 ZILIZOTOLEWA NA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR,