TANGAZO KWA MAIMAMU WOTE WA ZANZIBAR.
Posted: 2020-03-09 05:18:47
Assalama alaikum
Ofisi ya Mufti wa Zanzibar INAWAJUILISHA MAIMAMU WOTE kuwa wanaombwa walete Qunuti katika salaa ili Allah atunusuru na janga hili la maradhi haya ya Corona yalioingia takriban ulimwenguni kote.
Pia ofisi ya Mufti wa Zanzibar katika kikao chake na waandishi wa habari iliwasisitiza wananchi wote kufuata miongozo na maelekezo ya wataalamu wa afya katika kuchukua tahadhari juu ya maradhi haya ya Corona "hasa katika kipindi hichi" ikiwemo kuwacha kupeana mikono na badili yake wasalimiane kwa kauli tuu.