Wizara ya Katiba na Sheria imeundwa mnamo tahere 3/3/2019, baada ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein, kufanya maamuzi ya kuigawa Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kufanya Wizara mbili. Kutokana na Mgawanyiko huo, Wizara ya Katiba na Sheria inayo majukumu Yafuatayo:
- Kuandaa na kusimamia mipango, sera, sheria na tafiti zinazohusiana na Katiba na Sheria
- Kusimamia shughuli za utawala, uendehaji na utumishi katika Wizara
- Kusimamia utekelezaji wa Katiba ya Zanzibarna ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania
- Kusimamia Shughuli za Mhimili wa Mahakama
- Kusimamia shughuli za Ofisi ya Mwanasheria Mkuu
- Kusimamia shughuli za Mkurugenzi wa Mashtaka
- Kusimamia shughuli za Tume ya Kurekebisha Sheria
- Kuratibu na kusimamia shughuli za ofisi za Mufti
- Kuratibu na kusimamia shughuli za kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana
- Kuratibu shughuli za Wizara Pemba
Kutoa huduma bora kwa jamii kwa kuzingatia misingi ya Katiba, sheria, haki, demokrasia na utawala bora.
Kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora kwa jamii zenye ufanisi na tija kwa kuzingatia misingi ya Katiba na Sheria, haki za binadamu ili kuwa na Mfumo Madhubuti wa Kufanikisha Mipango ya Maendeleo ya Taifa
- Umoja katika utoaji wa huduma
- Kutokuwa na ubinafsi katika utoaji wa huduma
- Uadillifu/ uaminifu
- Kuzingatia haki/utii wa sheria
- Kuzingatia masuala ya jinsia
- Mashirikiano, uwajibikaji na uwazi
- Ufanisi na tija
- Huduma bora na kuwajalii wataka huduma
- Kuzingatia matokeo
- Thamani halisi ya pesa (value for money)
- Utunzaji wa siri
Wizara ya Katiba na Sheria inaundwa na Taasisi zifuatazo:-
- Idara ya Msaada wa Kisheria(Department of Legal Aid Services)
- Idara ya Uendeshaji na Utumishi (Department of Administration and Personnel)
- Idara ya Sera, Mipango na Utafiti (Department of Policy, Planning and Research)
- Ofisi Kuu Pemba
- Ofisi ya Mufti wa Zanzibar
- Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana
- Kitengo cha Hesabu
- Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
- Kitengo cha Ugavi na Ununuzi
- Kitengo cha Mawasiliano na Umma
- Kitengo cha TEHAMA