Head image
Govt. Logo

Hits 38534 |  1 online

     
IDARA NA VITENGO VYA WIZARA

Majukumu ya Wizara yamegawika kulingana na muundo wake, kila Idara/Kitengo hufanya majukumu maalum iliyopangiwa kama ifuatavyo:

IDARA YA MSAADA WA KISHERIA

Madhumuni

Kuratibu,kuendesha na kusimamia utoaji wa msaada wa kisheria.

Kazi za Idara

  1. Kutoa miongozo ya kisera kwa wotoaji wa msaada wa kisheria;
  2. Kumshauri Waziri kuhusu sera na mambo mengine muhimu yanayohusu kuimarisha utoaji wa msaada wa kisheria;
  3. Kusajili watoaji wa msaada wa kisheria;
  4. Kuweka na kutunza daftari la watoaji msaada wa kisheria,na kuweka kumbukumbu na taarifa zinazohusiana na watoaji wa msaada wa kisheria;
  5. Kumtaka mtoa msaada wa kisheria kutoa huduma ya msaada wa kisheria kwa mtu asiyekuwa na uwezo;
  6. Kupokea na kujumuisha ripoti za robo mwaka kuhusiana na huduma za msaada wa kisheria kutoka kwa watoaji msaada wa kisheria;
  7. Kutayarisha taarifa mbalimbali kuhusu huduma za msaada wa kisheria na mambo mengine kwa ajili ya kuwasilisha mbele ya Katibu Mkuu;
  8. Kurahisisha ubadilishanaji wa taarifa katika mfumo unaorahisisha upatikanaji wa taarifa hizo na kutoa miongozo kwa ajili ya ushirikiano na mawasiliano baina ya watoaji wa msaada wa kisheria na Serikali;
  9. Kuratibu, kufuatilia na kutathmini kazi za watoaji wa msaada wa kisheria na kutoa maelekezo ya jumla kwa ajili ya utekelezaji unaofaa wa program za msaada wa kisheria katika kiwango kilichowekwa na ubora wa huduma za msaada wa kisheria;
  10. Kupokea na kujumuisha taarifa za mwaka za watoaji wa msaada wa kisheria;
  11. Kuratibu na kurahisisha utengenezaji na uidhinishaji wa mtaala kwa ajili ya mafunzo ya wasaidizi wa sheria kwa kushauriana na watoaji wa msaada wa kisheria na taasisi za elimu na taasisi za mafunzo;
  12. Kushajihisha na kuwezesha utatuzi wa migogoro kupitia njia mbadala za utatuzi wa migogoro;
  13. Kuchukua hatua zinazofaa kuimarisha elimu ya sheria na uelewa wa kisheria miongoni mwa jamii na, hususan,kuelimisha makundi maalum kuhusu upatikanaji wa msaada wa kisheria;
  14. Kuanzisha na kuendeleza program kwa ajili ya elimu ya msaada wa kisheria na mafunzo na utoaji vyeti kwa wasaidizi wa sheria;
  15. Na kupokea na kupeleleza malalamiko na tabia mbaya dhidi ya watoaji wa msaada wa kisheria;

Idara hii imegawika katika sehemu kuu mbili, nazo ni

  • Sehemu ya Ufuatiliaji na Uratibu wa Msaada wa Kisheria

    Majukumu

    1. Kufanya tafiti kuhusu mapendekezo ya kisera yanayohusiana na utoaji wa msaada wa kisheria;
    2. Kuratibu na kurekebisha utoaji wa msaada wa kisheria, watoa msaada wa kisheria na kutayarisha mfumo na taarifa zinazohusiana na msaada wa kisheria;
    3. Kuchambua mikataba ya kikanda na kimataifa kuhusu utekelezaji wa haki za kisheria;
    4. Kupokea, kuchambua, kuchunguza na kushughulikia malalamiko katika utoaji wa huduma za kisheria;
    5. Kufanya tafiti kutambua na kuchunguza maeneo yenye udhaifu katika ufikishwaji wa huduma za haki, kutayarisha na kutekeleza mbinu za kupunguza/kuondosha malalamiko hayo;
    6. Kushauri juu ya masuala ya kisheria kuhusiana na ukatilidhidi ya wanawake na watoto; na
    7. Kuratibu na kutoa taarifa juu ya utekelezaji wa ICGLR
  • Sehemu ya Uratibu na Ufuatiliaji wa Masuala ya Haki za Binadamu

    Majukumu

    1. Kuandaa na kuendeleza sera pana ya utekelezaji wa haki za Binadamu
    2. Kuweka mikakati ya kuongoza taifa katika utekelezaji wa majukumu ya haki za Binadamu
    3. Kusimamia uendelezaji wa misingi ya haki za Binadamu
    4. Kushirikisha Ofisi za Mwanasheria Mkuu na Wakili Mkuu kwenye mashauriano ya masuala ya Haki za Binadamu.
    5. Kufanya mapitio ya sheria za ndani ili kuhakikisha uwepo wa uzingatiaji wa miongozo ya Ukanda na ya Kimataifa kuhusu haki za Binadamu.
    6. Kuhamasisha watumishi wa umma kushiriki katik kuimarisha masuala ya haki za binadamu.

IDARA YA UENDESHAJI NA UTUMISHI

Madhumuni

Kutoa huduma za kitaalam za utawala, uendeshaji na usimamizi wa rasilimali watu ya Wizara.

Kazi za Idara

  1. Kutoa ushauri wa kimkakati wa uendeshaji na usimamizi wa rasilimali watu yakiwemo ajira, maendeleo ya rasilimali watu, mafunzo, nidhamu, ubakizaji watumishi, usimamizi wa utendaji, na maslahi wa watumishi.
  2. Kuhakikisha matumizi sahihi, na usimamizi wenye ufanisi wa rasilimali watu kwenye Wizara.
  3. Kukusanya, Kuchambua, kuhifadhi, taarifa za rasilimali watu, na kusambaza taarifa za mipango ya maendeleo ya rasilimaki watu
  4. Kutoa ushauri kwa Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu maudhui na matumizi ya Sera ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Sheria za Utumishi wa Umma,
  5. Kutoa takwimu na taarifa mbali mbali za rasilimali watu za wakati uliopo
  6. Kutoa hududma za kiutawala na maendeleo ya kitaasisi.
  7. Kuandaa na kushughulikia mafao ya watumishi wanaoacha kazi.
  8. Kutoa ushauri kwa Katibu Mkuu kuhusu mambo ya rasilimali watu
  9. Kutafsiri na kuhakikisha ufanisi katika utekelezaji wa shughuli mbali mbali zinazoagizwa na mamlaka mbalimbali

Idara hii imegawika katika sehemu kuu mbili, nazo ni

  • Sehemu ya Utawala na Uendeshaji

    Majukumu

    1. Kutafsiri na kuhakikisha uzingatiaji wa Kanuni za Utumishi wa Umma, Kanuni za Kudumu na sheria za Kazi.
    2. Kuwezesha uwepo wa mahusiano stahili miongoni mwa watumishi.
    3. Kusimamia masuala yote ya itifaki
    4. Kusimamia huduma za ulinzi, usafirishaji na usafi wa mazingira
    5. Kusimamia huduma za vifaa vya ofisi, matengenezo ya majengo, na usafi wa ofisi.
    6. Kuratibu uzingatiaji wa maadili na thamani ya heshima Wizarani
    7. Kusimamia uzingatiaji wa masuala mtambuka kama vile jinsia, watu wenye ulemavu, VVU / UKIMWI na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
    8. Kuratibu utekelezaji wa ushirikishwaji wa sekta binafsi katika wizara.
    9. Kuratibu maandalizi na utekelezaji wa bajeti ya Mwaka ya Idara ya Utawala.
    10. Kuratibu utekelezaji wa mkakati wa kuinua kiwango cha utendaji wa ndani ya wizara.
    11. Kutoa ushauri wa kuinua ufanisi wa miundo ya ndani ya wizara
    12. Kuratibu utekelezaji wa Mktaba wa Huduma kwa Mteja kwa Wizara (Client Service Charter)
  • Sehemu ya Usimamizi wa Rasilimali watu

    Majukumu

    1. Kuratibu ajira na uteuzi ya watumishi wapya, upangaji watumishi, kuthibitishwa kazini, upandishwaji vyeo, na uhamisho ndani ya wizara
    2. Kutoa huduma za Masjala, Utarishi, na Kumbukumbu za Ofisi.
    3. Kuandaa Mpango wa Rasilimali watu na kutambua mahitaji ya wataalamu ya Wizara
    4. Kusimamia maandalizi na malipo ya mishahara
    5. Kuratibu utekelezaji wa Mfumo wa Wazi wa Upimaji Utendaji Kazi, kutathmini matokeo ya upimaji, kuandaa taarifa, na kufuatilia utekelezaji wa matokeo ya upimaji.
    6. Kushughulikia likizo mbali mbali za watumishi
    7. Kuandaa mafao na stahili za watumishi wanaoondoka kazini
    8. Kuandaa makisio ya mishahara na posho za watumishi za mwaka.
    9. Kuandaa na kuwezesha utekelezaji wa mpango wa mfululizo wa kurithishana ndani ya Wizara.
    10. Kuwezesha mafunzo kazini kwa watumishi wapya wa Wizara.
    11. Kuendesha tathmini ya mahitaji ya mafunzo kwa watumishi, mpango wa mafunzo, na kufuatilia utekelezaji wake ndani ya wizara.
    12. Kutekeleza jukumu la huduma za Sekreterieti ya Kamati ya Ajira na Maendeleo ya Watumishi ya Wizara.
    13. Kupokea, kuchambua na kuratibu taarifa mbalimbali zinazohusu rasilimali watu ndani ya wizara na taasisi zake.

IDARA YA SERA, MIPANGO NA UTAFITI

Madhumuni

Kutoa huduma za utaalamu za ushauri katika utungaji na uandaaji wa sera, mipango, na kuongoza kazi ya tathmini na ufuatiliaji kwenye Wizara.

Kazi za Idara

  1. Kuratibu maandalizi ya sera za kisekta, kufuatilia utekelezaji na kufanya tathmini ya athari zake.
  2. Kuchambua sera za sekta nyingine na kutoa ushauri ipasavyo
  3. Kuratibu maandalizi na utekelezaji wa Mipango na Bajeti ya Wizara na kufanya tathmini na ufuatiliaji wa mipango na Bajeti hizo
  4. Kutekeleza Mipango ya udhibiti wa athari (risk management plan)
  5. Kufanya tafiti, tathmini na ufuatiliaji wa mipango ya Wizara.
  6. Kuhamasisha na kuwezesha upatikanaji wa hududma za sekta binafsi Wizarani
  7. Kuratibu michango ya Wizara kwa Hotuba ya Bajeti na Ripoti ya Uchumi ya Mwaka.
  8. Kurasimisha uandaaji wa mipango ya kimkakati, bajeti, tathmini na ufuatiliaji wizarani.
  9. Kufanya tatfiti na chambuzi za kina kwenye sekta ya sheria na kutambua maeneo yanayohitaji kuwekewa sera
  10. Kuandaa mipango ya sekta ya sheria ya muda mfupi na mrefu

Idara hii imegawika katika sehemu kuu mbili, nazo ni

  • Sehemu ya Uratibu wa Sera na Tafiti

    Majukumu

    1. Kuandaa, kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa sera za Wizara
    2. Kuchambua na kutoa ushauri kwa sera zinazotungwa na wizara nyingine.
    3. Kufanya utafiti wa athari za sera mbalimbali na kutoa ushauri wa namna ya kuzifanyia kazi
    4. Kuratibu uandaaji na kufanya mapitio ya sera za Kiwizara
    5. Kushiriki uchambuzi wa shughuli (zisizo za msingi wizarani) ambazo zinaweza kufanywa na asasi za nje (outsourcing) na ushirikishwaji wa sekta binafsi na kuliwekea sera stahili
    6. Kutafsiri na kuhakikisha ufanisi katika utekelezaji wa sera mbali mbali zinazoagizwa na mamlaka mbalimbali
    7. Kupokea kuchambua na kuratibu maoni ya wadau na kuandaa mapendekezo ya uundaji ama marekebisho ya sera mbalimbali kutoka sekta ama taasisi husika.
    8. Kufanya tafiti na kutoa mapendekezo ya sera kwa masuala ya sekta na sheria.
  • Sehemu ya Mipango, Tathmini na Ufuatiliaji

    Majukumu

    1. Kuratibu uandaaaji wa Mpango Mkakati wa muda wa Kati, na Mipango ya utekelezaji ya mwaka na Bajeti
    2. Kuratibu na kuandaa Hotuba ya Bajeti ya Wizara
    3. Kukusanya taarifa za utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi na za Kamati za Bunge
    4. Kukusanya Taarifa za Miradi ya Wizara, Programu na kutengeneza mikakati ya upatikanaji wa rasilimali.
    5. Kushirikisha Wizara ya Fedha na OR Utumishi wa Umma kwenye mchakato wa utengenezaji Mpango Mkakati na Bajeti
    6. Kukusanya Taarifa za Miradi ya Wizara na Programu, na kutengeneza mikakati ya upatikanaji wa rasilimali.
    7. Kutoa maelekezo ya kitaalam katika kurasimisha uundaji wa Mpango Mkakati na bajeti kwa Idara za ndani ya Wizara.
    8. Kushiriki uchambuzi wa shughuli(zisizo za msingi wizarani) zinazo stahili kufanywa na asasi za nje ya serikali (outsourcing) na ushirikishwaji wa sekta binafsi

MAJUKUMU YA OFISI KUU PEMBA

Kuratibu na kusimamia shughuli zote za Wizara ya Katiba na Sheria kwa upande wa Pemba.

KITENGO CHA UHASIBU

Madhumuni

Kutekeleza majukumu ya usimamizi wa mifumo ya fedha kwa mujibu wa taratibu zinazo zingatia maadili na kutoa huduma zenye kiwango za utunzaji mahesabu.

Kazi za Kitengo

  1. Mishahara
    • Kuandaa malipo ya mishara na makto ya kisheria.
    • Kusimamia msihahara
    • Kusimamia bajeti ya mishahara na stahili za watumishi
    • Kutunza kumbukumbu za mahesabu
  2. Ofisi ya Malipo

    Kuwasilisha Ankara za malipo / kusimamaia hundi toka Hazina/ Ripoti za Fedha nk

  3. Ofisi ya Mapato
    • Kukusanya na kutunza kumbukumbu za mapato
    • Usulishi wa Benki nk
  4. Pencheni
  5. Bajeti
  6. Ukaguzi wa Ndani

KITENGO CHA UKAGUZI WA NDANI

Madhumuni

Kutoa huduma za uhakiki wa uhalisia wa thamani ya fedha (value for money) na matumizi sahihi ya na yenye ufanisi kwenye matumizi ya rasilimali za umma.

Kazi za Kitengo

  1. Mapitio ya Taarifa za udhibiti wa matumizi
  2. Mapiutio na uhakiki wa uzingatiaji taratibu na mifumo ya kisherai ya fedha
  3. Ukaguzi wa Miiradi
  4. Mpango wa udhibiti wa mwaka – Annual Audit Plan

KITENGO CHA UGAVI NA MANUNUZI

Madhumuni

Kutoa huduma na kitaalam katika manunuzi, utunzaji na ugawaji wa bidhaa na huduma katika Wizara.

Kazi za Kitengo

  1. Kutoa ushauri kwenye manunuzi ya huduma an bidhaa kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi
  2. Endeleza Mpango wa Manunuzi
  3. Kufanya manunuzi, ugavi, wa bidhaa na huduma
  4. Kusimamia ununuzi wowote na uuzaji wa mali za Wizara kwa njia ya Zabuni isipokuwa usuluhishi na kutunuku zabuni
  5. Kuratibu shughuli za Bodi ya Zabuni ya Wizara
  6. Kutekeleza maamuzi ya Bodi ya Zabuni ya Wizara
  7. Kufanya kazi kama Sekritarieti ya Bodi ya Zabuni ya Wizara
  8. Kuandaa mpango wa Ununuzi na Uuzaji wa mali za Wizara kwa njia ya Zabuni
  9. Kupendekeza ununuzi na uondoshaji wa mali za Wizara kwa utaratibu wa zabuni
  10. Kukagua na kuainisha upungufu wa mahitaji katika Wizara na kutoa tamko kuhusu mahitaji hayo
  11. Kuandaa nyaraka za zabuni kwa ajili wazabuni kushiriki
  12. Kuandaa matangozo ya fursa za zabuni
  13. Kuandaa rasmu za Mikataba
  14. Kutoa mikataba iliyothibitishwa na kusainiwa
  15. Kuandaa na kuhifadhi kumbukumbu za mchakato wa ununuzi na uuzaji wa mali za Wizara
  16. Kuandaa na kutunza orodha au kitabu cha mikataba yote ambayo Wizara imetunuku
  17. Kuandaa taarifa za kila mwezi kwa ajili ya Bodi ya Zabuni ya Wizara
  18. Kuandaa taarifa ya kila robo ya mwaka juu ya utekelezaji wa mpango wa ununuzi na kuwasilisha katika kikao cha menejimenti ya Wizara
  19. Kuratibu kazi za ununuzi na uondoshaji wa mali za serikali katika Idara na vitengo vyote vya Wizara; na
  20. Kuandaa taarifa nyinginezo kadri zitakavyo hitajika muda wowote.

KITENGO CHA MAWASILIANO NA UMMA

Madhumuni

Kuratibu uzalishaji, usambazji na uelimishaji wa habari za huduma za sheria kwa madhumuni ya kuweka mazingira sahihi ya uelewa, na mitazamo kwa wadau na jamii kuhusu mifumo ya sheria na taswira ya SMZ.

Kazi za Kitengo

  1. Kusimamia na kuratibu kazi za Idara, kutayarisha bajeti ya idara, kushiriki vikao vya menejimenti
  2. Kuratibu kazi za maendeleo katika sekta ya habari
  3. Kuratibu habari za Wizara na kuzitoa kwa wahusika kwa mujibu wa kanuni
  4. Kusimamia utafiti wa habari
  5. Kutoa ushauri wa kitaalamu katika fani ya habari kwa viongozi wakuu
  6. Kutoa ushauri wa kitaalamu katika fani ya habari kwa taasisi zilizo chini ya wizara
  7. Kushiriki mijadala mbalimbali na vyombo vya habari kuhusu masuala yanayohusu wizara
  8. kuisemea wizara
  9. kusimamia na kubadilidha taarifa za katika tovuti na mitandao ya kijamii

KITENGO CHA TEKNOLOJIA HABARI NA MIFUMO YA MAWASILIANO

Madhumuni

Kutoa huduma na utaalam kwenye mikakati na malengo ya Wizara kupitia matumizi yenye kiwango na uhakika ya mifumo ya Habari na mwasiliano ndani ya wizara.

Kazi za Kitengo

  1. Kutekeleza sera ya TEHAMA na serikali –mfumo (e-Government strategy);
  2. Kuendeleza kutekeleza na masuala ya TEHAMA pamoja na Sera ya Serikali Mtandao (e-Government Policy) Wizarani
  3. Kuratib uwajishwaji na Uwendelezaji wa mkakati wa Mfumo wa Teknojia ya Habari na Mawasiliano
  4. Kushauri Uongozi wa Ofisi juu ya Matumizi Mazuri ya vifaa vya TEHAMA na PROGRAMU zake
  5. Kuratib maendeleo ya uhifadhi wa program katika kuhakikisha usalama wa Taarifa za ofisi
  6. Kuhakikisha kuwa vifaa vya TEHAMA na programu zake zinatunzwa ipasavyo
  7. Kuratibu na kutoa ushauri wa manunuzi ya vifaa na programu za TEHAMA
  8. Kuanzisha na kuratibu matumizi ya Mawasiliano ya kielekitroniki kwenye Local Area Network (LAN) na Wide Area Network (WAN)
  9. Kufanya utafiti na kushauri maeneo ambayo TEHAMA inaweza kutumika ili iwe chombo cha kuhuisha utoaji wa huduma Wizarani.

Huduma za Tehama

Barua Pepe Msaada wa kisheria

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

MAHAKAMA DPP WAKFU LRC SADC IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 772, Mazizini, Zanzibar
Tel.: +255(24)2234683 Mhe Waziri



Tel.: +255 (24)2234684 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2234689
Email: info@sheriasmz.go.tz