IDARA YA SERA, MIPANGO NA UTAFITI
Madhumuni
Kutoa huduma za utaalamu za ushauri katika utungaji na uandaaji wa sera, mipango, na kuongoza kazi ya tathmini na ufuatiliaji kwenye Wizara.
Kazi za Idara
- Kuratibu maandalizi ya sera za kisekta, kufuatilia utekelezaji na kufanya tathmini ya athari zake.
- Kuchambua sera za sekta nyingine na kutoa ushauri ipasavyo
- Kuratibu maandalizi na utekelezaji wa Mipango na Bajeti ya Wizara na kufanya tathmini na ufuatiliaji wa mipango na Bajeti hizo
- Kutekeleza Mipango ya udhibiti wa athari (risk management plan)
- Kufanya tafiti, tathmini na ufuatiliaji wa mipango ya Wizara.
- Kuhamasisha na kuwezesha upatikanaji wa hududma za sekta binafsi Wizarani
- Kuratibu michango ya Wizara kwa Hotuba ya Bajeti na Ripoti ya Uchumi ya Mwaka.
- Kurasimisha uandaaji wa mipango ya kimkakati, bajeti, tathmini na ufuatiliaji wizarani.
- Kufanya tatfiti na chambuzi za kina kwenye sekta ya sheria na kutambua maeneo yanayohitaji kuwekewa sera
- Kuandaa mipango ya sekta ya sheria ya muda mfupi na mrefu
Idara hii imegawika katika sehemu kuu mbili, nazo ni
Sehemu ya Uratibu wa Sera na Tafiti
Majukumu
- Kuandaa, kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa sera za Wizara
- Kuchambua na kutoa ushauri kwa sera zinazotungwa na wizara nyingine.
- Kufanya utafiti wa athari za sera mbalimbali na kutoa ushauri wa namna ya kuzifanyia kazi
- Kuratibu uandaaji na kufanya mapitio ya sera za Kiwizara
- Kushiriki uchambuzi wa shughuli (zisizo za msingi wizarani) ambazo zinaweza kufanywa na asasi za nje (outsourcing) na ushirikishwaji wa sekta binafsi na kuliwekea sera stahili
- Kutafsiri na kuhakikisha ufanisi katika utekelezaji wa sera mbali mbali zinazoagizwa na mamlaka mbalimbali
- Kupokea kuchambua na kuratibu maoni ya wadau na kuandaa mapendekezo ya uundaji ama marekebisho ya sera mbalimbali kutoka sekta ama taasisi husika.
- Kufanya tafiti na kutoa mapendekezo ya sera kwa masuala ya sekta na sheria.
Sehemu ya Mipango, Tathmini na Ufuatiliaji
Majukumu
- Kuratibu uandaaaji wa Mpango Mkakati wa muda wa Kati, na Mipango ya utekelezaji ya mwaka na Bajeti
- Kuratibu na kuandaa Hotuba ya Bajeti ya Wizara
- Kukusanya taarifa za utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi na za Kamati za Bunge
- Kukusanya Taarifa za Miradi ya Wizara, Programu na kutengeneza mikakati ya upatikanaji wa rasilimali.
- Kushirikisha Wizara ya Fedha na OR Utumishi wa Umma kwenye mchakato wa utengenezaji Mpango Mkakati na Bajeti
- Kukusanya Taarifa za Miradi ya Wizara na Programu, na kutengeneza mikakati ya upatikanaji wa rasilimali.
- Kutoa maelekezo ya kitaalam katika kurasimisha uundaji wa Mpango Mkakati na bajeti kwa Idara za ndani ya Wizara.
- Kushiriki uchambuzi wa shughuli(zisizo za msingi wizarani) zinazo stahili kufanywa na asasi za nje ya serikali (outsourcing) na ushirikishwaji wa sekta binafsi