Head image
Govt. Logo

Hits 35456 |  12 online

     

IDARA YA MSAADA WA KISHERIA

Madhumuni

Kuratibu,kuendesha na kusimamia utoaji wa msaada wa kisheria.

Kazi za Idara

  1. Kutoa miongozo ya kisera kwa wotoaji wa msaada wa kisheria;
  2. Kumshauri Waziri kuhusu sera na mambo mengine muhimu yanayohusu kuimarisha utoaji wa msaada wa kisheria;
  3. Kusajili watoaji wa msaada wa kisheria;
  4. Kuweka na kutunza daftari la watoaji msaada wa kisheria,na kuweka kumbukumbu na taarifa zinazohusiana na watoaji wa msaada wa kisheria;
  5. Kumtaka mtoa msaada wa kisheria kutoa huduma ya msaada wa kisheria kwa mtu asiyekuwa na uwezo;
  6. Kupokea na kujumuisha ripoti za robo mwaka kuhusiana na huduma za msaada wa kisheria kutoka kwa watoaji msaada wa kisheria;
  7. Kutayarisha taarifa mbalimbali kuhusu huduma za msaada wa kisheria na mambo mengine kwa ajili ya kuwasilisha mbele ya Katibu Mkuu;
  8. Kurahisisha ubadilishanaji wa taarifa katika mfumo unaorahisisha upatikanaji wa taarifa hizo na kutoa miongozo kwa ajili ya ushirikiano na mawasiliano baina ya watoaji wa msaada wa kisheria na Serikali;
  9. Kuratibu, kufuatilia na kutathmini kazi za watoaji wa msaada wa kisheria na kutoa maelekezo ya jumla kwa ajili ya utekelezaji unaofaa wa program za msaada wa kisheria katika kiwango kilichowekwa na ubora wa huduma za msaada wa kisheria;
  10. Kupokea na kujumuisha taarifa za mwaka za watoaji wa msaada wa kisheria;
  11. Kuratibu na kurahisisha utengenezaji na uidhinishaji wa mtaala kwa ajili ya mafunzo ya wasaidizi wa sheria kwa kushauriana na watoaji wa msaada wa kisheria na taasisi za elimu na taasisi za mafunzo;
  12. Kushajihisha na kuwezesha utatuzi wa migogoro kupitia njia mbadala za utatuzi wa migogoro;
  13. Kuchukua hatua zinazofaa kuimarisha elimu ya sheria na uelewa wa kisheria miongoni mwa jamii na, hususan,kuelimisha makundi maalum kuhusu upatikanaji wa msaada wa kisheria;
  14. Kuanzisha na kuendeleza program kwa ajili ya elimu ya msaada wa kisheria na mafunzo na utoaji vyeti kwa wasaidizi wa sheria;
  15. Na kupokea na kupeleleza malalamiko na tabia mbaya dhidi ya watoaji wa msaada wa kisheria;

Idara hii imegawika katika sehemu kuu mbili, nazo ni

  • Sehemu ya Ufuatiliaji na Uratibu wa Msaada wa Kisheria

    Majukumu

    1. Kufanya tafiti kuhusu mapendekezo ya kisera yanayohusiana na utoaji wa msaada wa kisheria;
    2. Kuratibu na kurekebisha utoaji wa msaada wa kisheria, watoa msaada wa kisheria na kutayarisha mfumo na taarifa zinazohusiana na msaada wa kisheria;
    3. Kuchambua mikataba ya kikanda na kimataifa kuhusu utekelezaji wa haki za kisheria;
    4. Kupokea, kuchambua, kuchunguza na kushughulikia malalamiko katika utoaji wa huduma za kisheria;
    5. Kufanya tafiti kutambua na kuchunguza maeneo yenye udhaifu katika ufikishwaji wa huduma za haki, kutayarisha na kutekeleza mbinu za kupunguza/kuondosha malalamiko hayo;
    6. Kushauri juu ya masuala ya kisheria kuhusiana na ukatilidhidi ya wanawake na watoto; na
    7. Kuratibu na kutoa taarifa juu ya utekelezaji wa ICGLR
  • Sehemu ya Uratibu na Ufuatiliaji wa Masuala ya Haki za Binadamu

    Majukumu

    1. Kuandaa na kuendeleza sera pana ya utekelezaji wa haki za Binadamu
    2. Kuweka mikakati ya kuongoza taifa katika utekelezaji wa majukumu ya haki za Binadamu
    3. Kusimamia uendelezaji wa misingi ya haki za Binadamu
    4. Kushirikisha Ofisi za Mwanasheria Mkuu na Wakili Mkuu kwenye mashauriano ya masuala ya Haki za Binadamu.
    5. Kufanya mapitio ya sheria za ndani ili kuhakikisha uwepo wa uzingatiaji wa miongozo ya Ukanda na ya Kimataifa kuhusu haki za Binadamu.
    6. Kuhamasisha watumishi wa umma kushiriki katik kuimarisha masuala ya haki za binadamu.

Huduma za Tehama

Barua Pepe Msaada wa kisheria

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

MAHAKAMA DPP WAKFU LRC SADC IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 772, Mazizini, Zanzibar
Tel.: +255(24)2234683 Mhe Waziri



Tel.: +255 (24)2234684 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2234689
Email: info@sheriasmz.go.tz