Hits 86464 | 4 online
WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA MHE KHAMIS JUMA MWALIM
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Khamis Juma Mwalim amemshukuru na kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dkt Ali Mohamed Shein kwa maelekezo yaliyowezesha kuinua utendaji katika Wizara ya Katiba na Sheria, pamoja muongozo mzuri uliopelekea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015 - 2020 jambo ambalo Wizara ya Katiba na Sheria inajivunia kutekeleza kwa mafanikio makubwa Ibara ya 121 (d) na (e). “ Hakika umuhimu wa Sekta ya Sheria kwa wananchi umeonekana kupitia maonesho ya Wiki ya Sheria ambapo wananchi walijitokeza kwa wingi kujifunza, kupata maelekezo na hata kuelezea shida zao za kisheria kwa watendaji wetu waliokuwa tayari kuwahudumia”aliongezea Waziri Khamis .