Head image
Govt. Logo

Hits 70255 |  3 online

     
Katibu Mkuu Wizaraya Katiba na Sheria Ndg George Joseph Kazi amewataka wasaidizi wa sheria kutafuta njia mbadala za kusuluhisha migogoro na kuacha kukimbilia mahakaman
news phpto

Katibu Mkuu Wizaraya Katiba na Sheria Ndg George Joseph Kazi amewataka wasaidizi wa sheria kutafuta njia mbadala za kusuluhisha migogoro na kuacha kukimbilia mahakaman

Katibu Mkuu Wizaraya Katiba na Sheria Ndg George Joseph Kazi amewaka wasaidizi wa sheria kutafuta njia mbadala za kusuluhisha migogoro na kuacha kukimbilia mahakamani badala yake kutumia njia nzuri ya kuwakutanisha watu pamoja na kufanya mazungumzo yenye nia ya kumaliza tatizo kiusalama na kwa maridhiano

“tunaweza kuipunguzia Serikali gharama zisizo na msingi sio kila kesi kukimbilia Polisi au Mahakamani wasaidizi wa sheria fanyeni kazi zenu itumikieni jamii wasikilizeni matatizo yao na muwape ushauri mzuri ili jamii izidi kuwa na Imani juu yenu”

Ingawa yapo matatizo inawezekana hayawezi kuishia hapo yanakwenda mahakamani ni vyema kujifunza ili kufahamu kesi za madai na maeneo yaliyoruhusiwa

Mashauri yanayohusu watoto masuala ya kikatiba yale yanayohusu haki za msingi wa kibinaadamu kama haki ya kumiliki mali haki ya kuishi wasaidizi wa sheria wanapaswa kufahamu ili waweze kuelewa vizuri mipaka yao

Katibu George aliyasema hao wakati alipokuwa akiyafungua mafunzo ya wasaidizi wa sheria yenye lengo la kuwakumbusha umuhimu wa majukumu yao na mipaka yao kujuwa sheria na kanuni wakati wanapotoa huduma ya msaada wa sheria katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete Pemba .

Huduma za Tehama

Barua Pepe Msaada wa kisheria

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

MAHAKAMA DPP WAKFU LRC SADC IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 772, Mazizini, Zanzibar
Tel.: +255(24)2234683 Mhe WaziriTel.: +255 (24)2234684 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2234689
Email: info@sheriasmz.go.tz