Hits 40096 | 1 online
Mkurugenzi wa Idara ya Msaada wa Kisheria Bi Hanifa Ramadhan Said amesema kuwa kila mwananchi anayo haki ya kupata msaada wa kisheria bila ya ubaguzi kwa mujibu wa Sheria na Katiba ya Zanzibar
Mkurugenzi wa Idara ya Msaada wa Kisheria Bi Hanifa Ramadhan Said amesema kuwa kila mwananchi anayo haki ya kupata msaada wa kisheria bila ya ubaguzi kwa mujibu wa Sheria na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ambayo inasisitiza kulindwa kwa haki za binadamu
Ameyasema hayo kwenye mafunzo kwa wasaidizi wa sheria yaliyowakutanisha wasaidizi wa sheria kutoka Mkoa wa Kusini na Kaskazini Pemba kwenye ukumbi wa Makonyo Chake Chake .
Bi Hanifa amewahimiza wasaidizi wa sheria kuwa tayari kuitumia Idara ya Msaada wa Kisheria pamoja na maafisa wake kwa utaratibu maalum uliowekwa kwani sio watu wote watapewa huduma hio isipokuwa kwa yule asie na uwezo kama sheria na kanuni zinavyoelekezwa
“mafunzo yaliyotolewa yalete mabadiliko kwenu tusifanye kazi kwa mazowea tujitowe kwa jamii tukawasaidie na tuwape ushauri na nina imani kuona kuwa tutapata matokeo chanya ya mafunzo haya”