Head image
Govt. Logo

Hits 25082 |  4 online

     
Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar ameridhishwa na hatua za jengo jipya la mahakama kuu tunguu.
news phpto

Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar ameridhishwa na hatua za jengo jipya la mahakama kuu tunguu unaoendelea na kuwataka wakandarasi wa jengo hilo kuhakikisha wanajenga jengo lililobora na kumaliza kwa wakati kama ilivyokubaliwa katika mkataba.

Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mh, Khamis Juma Mwalim ameridhishwa na hatua zilizofikiwa za ujenzi wa Jengo jipya la Mahakama Kuu Tunguu na kuwataka wakandarasi hao kuhakikisha wanajenga Jengo lililobora na kumaliza kwa wakati kama ilivyo kubaliwa katika mkataba.

Akikagua ujenzi unaoendelea wa Jengo la Mahakama hiyo amesema changamoto iliyopo ya upungufu wa vifaa ni kutokana janga la maradhi ya Korona liliopo duniani kwa sasa na amewahakikishia wakandarasi hao kuwa vifaa vya ujezi wa Jengo hilo vitaingia nchini hivi karibuni hali itakaporuhusu ili kuhakikisha ujenzi unakamilika.

Aidha amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kuimarisha mfumo wa sheria kwa kujenga majengo mengine mapya ya Mahakama na kuyafanyia matengenezo yale ya zamani ili kuimarisha miundo mbinu ya kitaasisi na kiutendaji ya utoaji huduma na upatikanaji wa haki inapatikana kwa ufanisi.

Amesema ukiachana na Jengo jipya la Mahakama Kuu Tunguu pia Serikali tayari imeshajenga Jengo jipya la Mahakama ya watoto Mahonda na itaendelea kufannya hivyo ili kuimarisha sekta ya Mahakama nchini.

Akiyataja Majengo ambayo tayari yameshafanyiwa matengenezo makubwa ni pamoja Jengo la Mahakama Chakechake Pemba, Jengo la Mahakama ya Makunduchi, Jengo la Mahakama Mwera, na Jengo la Mahakama ya Mwanakwerekwe.

Nae mrajisi wa Mahakama kuu Zanzibar nd, Mohd Ali Mohd amewapongeza wakandarasi kwa jitihada waliyoionesha licha ya changamoto mbali mbali ikiwemo za mvua za masika na kuwataka kujenga katika hali ya ubora kwani wataendelea kusimamia mkataba ili kuhakikisha wanakwenda kwa mujibu wa makubaliano na kujenga kwa mujibu wa viwango vilivyowekwa.

Ujenzi huo hadi kumalizika kwake utaharimu karibu bilioni 16 za Tanzania kwa mujibu wa mkataba uliosainiwa.

Huduma za Tehama

Barua Pepe Msaada wa kisheria

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

MAHAKAMA DPP WAKFU LRC SADC IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 772, Mazizini, Zanzibar
Tel.: +255(24)2234683 Mhe WaziriTel.: +255 (24)2234684 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2234689
Email: info@sheriasmz.go.tz