Head image
Govt. Logo

Hits 32630 |  1 online

     
Wizara ya Katiba na Sheria Zanzibar imeandaa mikakati ambayo itahakikisha inawawezesha wasaidizi wa kisheria katika kuleta mafanikio ya utendaji wa kazi zao za kila siku.
news phpto

Wizara ya Katiba na Sheria Zanzibar imeandaa mikakati ambayo itahakikisha inawawezesha wasaidizi wa kisheria katika kuleta mafanikio ya utendaji wa kazi zao za kila siku.

Wizara ya Katiba na Sheria Zanzibar imeandaa mikakati ambayo itahakikisha inawawezesha wasaidizi wa kisheria katika kuleta mafanikio ya utendaji wa kazi zao za kila siku.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mipango Sera na Utafiti,Daima Mohammed Mkalimoto,wakati akifungua mafunzo kwa kuwakumbushia wasaidizi wa kisheria yaliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Malaria Mwanakwerekwe.

Daima alisema Wizara inaamini kwamba wasaidizi hao wamekua mstari wa mbele katika kuhakikisha inawapa elimu jamii ambayo imekubwa na matatizo mbali mbali na kuweza kujisaidia.

Alisema kuwa kuwepo kwao kumeweza kusaidia kupatikana mafanikio makubwa kwani jamii imeweza kuwatambua wasaidizi hao wa kisheria na kutatua matatizo mbali mbali yaliokuwa yakiwakabili.

“Ni ukweli kwamba Wizara ya Katiba imekuandalini mikakati ambayo itahakikisha mnafanya kazi zenu kwa ufanisi wa hali ya juu pamoja na kuleta maenedelea kwa jamii husika,”alisema.

Mkurugenzi huyo alitoa wito kwa wasaidizi hao wa mikoa mitatu ya Unguja kuhakikisha elimu watakayoipata waienzi na kuitumia inavyotakiwa kwa kuifikisha kwa jamii na kupatikane ufumbuzi wa matatizo yao.

Aidha Daima aliwataka washiriki hao wa mafunzo kuyasikiliza kwa umakini na kuyafahamu kutokana na mafunzo hayo kuwa ni chachu ya maendeleo ya msaada wa kisheria.

Nae Mkurugenzi wa Idara ya Mswaada wa Kisheria,Hanifa Ramadhani Said alisema awali wasaidizi wa kisheria walikuwa hawatambuliki katika jamii kutokana na jamii kutojua umuhimu wa watu hao.

Alisema hivi sasa jamii imekuwa mstari wa mbele kushirikiana nawasaidizi wa kisheria kutokana na kusaidiwa katika kutatuliwa matatizo yao mbali mbali yanayoleta mizozo katika familia.

“Napenda kutoa wito kwa washiriki wa mafunzo haya kuhakikisha wanaitumia taaluma watakayoipata ili wananchi wajue umuhimu wao katika sheria na kuitumia inavyotakiwa,”alisema.

Mratibu wa Legal Servicers Fercility(LFC) Joseph Shaaban Magazi alisema taasisi yake imeamua kuandaa mafunzo hayo kutokana na kuona jamii haifahamu umuhimu wa maswala ya kisheria na inahitaji kuelimishwa.

Alisema mnamo mwaka 2011 taasisi hiyo iliandaa mafunzo hayo ili kusaidia jamii kuepukana na matatizo mbali mbali yanayowakabili ya kisheria ikiwemo maswala ya ndoa,watoto pamoja na migogoro ya ardhi.

“Hii sio mara ya kwanza kufanya mafunzo haya tuliwahi kufanya mara ya mwanzo mwaka 2011 na hivi sasa tumeamua kurejea tena ili tuweze kuwakumbushia wasaidizi wa kisheria kufanya kazi kwa ufanisi kutokana na wengine kipindi hicho walikuwa hawapo,”. Alifafanua.

Nao washiriki wa mafunzo hayo walisema kwamba mafunzo hayo yatawasaidia katika kuwasaidia wananchi katika kutatua matatizo yao yanayowakabili kutokana na jamii kutojua maswala ya kisheria na kupata shida wakati wa kudai haki zao.

Mafunzo hayo ya siku tano ambayo yanafanyika katika Mikoa yote mitatu ya Unguja, huko Pemba yalifanyika mwezi wa Tatu yameadhaminiwa na LSF wakishirikiana na Idara ya Mswada wa Kisheria Zanzibar.

Huduma za Tehama

Barua Pepe Msaada wa kisheria

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

MAHAKAMA DPP WAKFU LRC SADC IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 772, Mazizini, Zanzibar
Tel.: +255(24)2234683 Mhe WaziriTel.: +255 (24)2234684 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2234689
Email: info@sheriasmz.go.tz