Head image
Govt. Logo

Hits 27778 |  3 online

     
Wizara ya Katiba na Sheria wakati ilipowasilisha Taarifa ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Mwaka 2019/2020 na Mpango Kazi wa mwaka 2020/2021.
news phpto

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameutaka uongozi wa Wizara ya Katiba na Sheria kuutumia vyema uzoefu na mafanikio uliyoyapata katika Awamu ya Saba ili uweze kufanya kazi vizuri katika Serikali ya Awamu ijayo.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameutaka uongozi wa Wizara ya Katiba na Sheria kuutumia vyema uzoefu na mafanikio uliyoyapata katika Awamu ya Saba ili uweze kufanya kazi vizuri katika Serikali ya Awamu ijayo.

Hayo aliyasema leo, Ikulu Jijini Zanzibar alipokutana na uongozi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakati ilipowasilisha Taarifa ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Mwaka 2019/2020 na Mpango Kazi wa mwaka 2020/2021.

Rais Dk. Shein aliwasisitiza viongozi wa Wizara hiyo kutorudi nyuma na badala yake waongeze kasi kwani sekta ya sheria imeweza kupata mafanikio makubwa hapa nchini ambayo yanafanana na yale yanayopatikana katika nchi nyengine zilizoendelea

Aliongeza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejitahidi kuweka mazingira mazuri katika sekta ya sheria, hivyo ni vyema sekta hiyo ikaendelea kuwatumikia wananchi ipasavyo.

Rais Dk. Shein alisema kuwa Awamu za uongozi katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimefuata Sheria na Katiba zilizopo ila pale inapotokea haja kufanywa marekebisho hufanywa kwa maslahi mazuri ya kuleta tija kwa nchi na wananchi wake.

Aidha, alieleza haja ya kuwafundisha wafanyakazi waliochini na kuwaelekeza ili waweze kuja kafanya kazi vizuri hapo baadae na kuwasisitiza kujiendeleza kimasomo kwani elimu ina umuhimu mkubwa na pia, ni jambo lililotukuka.

Rais Dk. Shein alisisitiza kuwa iwapo sekya ya elimu ikipewa kipaumbele Zanzibar itafika mbali kwani mataifa yote yaliopata mafanikio duniani yalilipa kipaumbe suala zima la elimu.

Rais Dk. Shein alisema kuwa bado Zanzibar inahitaji wasomi hivyo ni vyema watu wakasomeshana bila ya kufanyiana khiyana huku akisisitiza haja ya kushauriana ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa zaidi.

Rais Dk. Shein alieleza furaha yake kwa uongozi wa Wizara hiyo na kupokea shukurani na pongezi kubwa kutoka kwa uongozi huo ambazo zimetolewa kwa niaba na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Othman Ngwali.

Alisema kuwa sekta ya sheria imefanya kazi kubwa hapa nchini kwa kuchangia katika kuifikisha Zanzibar kuwa na Uchumi wa Kati kwani bila ya Sheria mafanikio hayo yasingelifikiwa hasa ikizingatiwa kwamba uchumi unakwenda sambamba na Utawala Bora.

Nae Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee alisema kuwa mikutano hiyo ya (Bango Kitita) imekuwa na msaada mkubwa katika Wizara za Serikali na kueleza haja ya kuendelezwa huku akisisitiza haja kwa viongozi na wafanyakazi wa Wizara hiyo kuendelea kuchapa kazi hasa katika kipindi hichi cha kuelekea uchaguzi mkuu ujao wa mwezi Oktoba mwaka huu.

Mapema Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria Khamis Juma Mwalim alitoa pongezi kwa Rais Dk. Shein kwa kuwaongoza vyema katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo Wizara hiyo inajivunia kutekeleza kwa mafanikio makubwa Ibara ya 121 (d) na (e).

Alisema uimarishaji wa Taasisi za Kisheria umepata msukumo mkubwa katika kipindi cha uongozi wa Dk. Shein kwa kuzitekeleza shughuli kadhaa zikiwemo za kufanyia mapitio sheria zilizopitwa na wakati, kuimarisha majengo ya Wizara, kuongeza idadi ya Majaji na Mahakimu hali iliyopelekea kuimarika kwa upatikanaji wa haki.

Waziri Mwalimu alitoa pongezi kwa Rais Dk. Shein pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli kwa kuiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa Kati pamoja na umahiri waliouonesha wakati dunia ilipokubwa na janga kubwa la Corona amabalo lilitikisa dunia na linaendelea kutikisa baadhi ya nchi duniani.

Alieleza kuwa kazi iloyofanywa na Tume ya kurekebisha Sheria ya kuzifanyia mapitio Sheria 22 kati ya Sheria 37 zimekamilika na kuwasilishwa katika Mamlaka husika ambapo kasi hiyo imechangia kuzifanyia mapitio sheria nane zinazohusu masuala ya ardhi ambapo ikikamilika itapelekea kupunguza kwa kiasi kikubwa migogoro ya ardhi na kuweka utaratibu bora wa matumizi na usimamizi wa ardhi.

Pia, Waziri huyo alieleza mambo mbali mbali yaliyotekelezwa na Wizara hiyo ikiwa ni pamoja na kuandaa Sheria mbali mbali ikiwemo Sheria ya Jumuiya ya Mawakili Zanzibar, Sheria ya Mawakili, Sheria ya Mufti na Sheria ya Skuli ya Sheria.

Aidha, alieleza kuwa ujenzi wa jengo la Mahakama Kuu Tunguu unaendelea vizuri ambapo hadi kufikia tarehe 30 Juni 2020 utekelezaji halisi ulifikia asilimia 55 wakati makadirio yake ni kufikia asilimia 65 ya ujenzi wote.

Waziri Mwalimu alieleza kuwa uratibu wa masuala ya kidini umeendelea ambapo Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana imeendelea na hatua za kuanzisha mfuko wa Hijja ambapo matarajio ni kuuzindua katika mwaka huu wa fedha.

Nao uongozi wa Wizara hiyo ulimpongeza Rais Dk. Shein kwa uongozi wake bora na kutoa shukurani kwa Rais Dk. Shein ambapo pia, walieleza jinsi wanavyojivunia kutokana na kuwezeshwa kwani sekta ya sheria haina tatizo ya vifaa wala bajeti huku wakimpongeza kwa kuiwacha Zanzibar ikiwa salama.

Uongozi huo ulieleza kuwa sekta ya Sheria imeimarika na Wanasheria wamekuwa na hadhi kubwa sana ikilinganisha na miaka ya nyuma ikiwa ni pamoja na kutungwa Sheria na kuwepo kwa Chuo cha Sheria cha kwenda kujifunza ambapo yote hayo yamepatikana

Huduma za Tehama

Barua Pepe Msaada wa kisheria

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

MAHAKAMA DPP WAKFU LRC SADC IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 772, Mazizini, Zanzibar
Tel.: +255(24)2234683 Mhe Waziri



Tel.: +255 (24)2234684 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2234689
Email: info@sheriasmz.go.tz