Head image
Govt. Logo

Hits 32622 |  1 online

     
Mkurugenzi wa Idara ya Msaada wa Kisheria Zanzibar Hanifa Ramadhan Said amesema wasaidizi wa sheria wana umuhimu mkubwa katika jamii
news phpto

Mkurugenzi wa Idara ya Msaada wa Kisheria Zanzibar Hanifa Ramadhan Said amesema wasaidizi wa sheria wana umuhimu mkubwa katika jamii kutokana na kazi zao katika msaada wa kisheria.

Mkurugenzi wa Idara ya Msaada wa Kisheria Zanzibar Hanifa Ramadhan Said amesema wasaidizi wa sheria wana umuhimu mkubwa katika jamii kutokana na kazi zao katika msaada wa kisheria.

Aliyasema hayo katika mkutano wa pili wa robo mwaka wa kuratibu masuala ya msaada wa kisheria uliofanyika ukumbi wa Wizara ya Habari,Utalii na Mambo ya Kale Kikwajuni Mjini Zanzibar.

Alisema jitihada hizo wanazozifanya wasaidizi wa sheria zinahitaji kutambuliwa na kuthaminiwa ili kuwapa hamasa ya kuenndeleza kufanya vizuri.

Alieleza kuwa sheria ya msaada wa sheria imewatambua wasaidizi wa sheria kama ni watoa msaada wa kisheria hivyo wanahitajika kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria na taratibu.

“Sera ya msaada wa kisheria ya mwaka 2017 katika hoja ya tatu inayojulikana upatikanaji mdogo wa huduma za msaada wa kisheria na watu maskini na wenye mahitaji maalum ambapo katika hoja hii moja ya mkakati wake wa pili ni kuimarisha mafunzo,utoaji wa vyeti, utambuzi na motisha kwa wasaidizi wa sheria” alisema Mkurugenzi huyo.

Aidha alieleza kuwa katika kuwajengea uwezo watoa huduma wa msaada wa kisheria na wataka huduma ili kurahisisha utekelezaji wa sheria ya msaada wa kisheria namba 13 ya mwaka 2018.

Akisoma ripoti ya mwaka ya utekelezaji wa shughuli za Idara ya Msaada wa Kisheria Afisa Sheria Ndugu Ali Haji alisema Idara hiyo imewafikia wananchi 338 wa Shehia nne za Unguja kwa kuwapa elimu ya kanuni na sheria za msaada wa kisheria na kwa Pemba wamewafikia wananchi 150 katika Wilaya ya Micheweni.

Alisema Idara pia imekamilishah kutayarisha mfumo wa usajili kwa njia ya kieliktroniki kwa ajili ya kuwasajili watoaji wa huduma wa kisheria.

Alisema mfumo huo kwa sasa unapelekea utambuzi wa watoaji msaada wa kisheria na kuiwezesha Serikali kupata takwlimu sahihi za watoa huduma za msaada wak isheria pamoja na wataka huduma hizo.

Aidha alieleza kwa kipindi cha mwaka idara inajivunia mafanikio mbalimbali ikiwemo kusimamia vizuri jukumu la kuratibu shughuli za msaada wa kisheria, kujenga ushirikiano wa karibu kati ya watoa huduma za msaada wa kisheria na wadau wengine na kukamilisha muongozo wa usajili wa watoa msaada wa kisheria.

Kwa upande wao washiriki wa Mkutano huo walisema kuwa saidizi wa sheria wanafanya kazi kubwa katika jamii lakini baadhi ya watu hawatoi ushirikiano kwao hali ambayo inawafanya kufanya kazi katika mazingira magumu.

Huduma za Tehama

Barua Pepe Msaada wa kisheria

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

MAHAKAMA DPP WAKFU LRC SADC IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 772, Mazizini, Zanzibar
Tel.: +255(24)2234683 Mhe WaziriTel.: +255 (24)2234684 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2234689
Email: info@sheriasmz.go.tz