Head image
Govt. Logo

Hits 35373 |  10 online

     
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(SMT) na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) zimejidhatiti kwa pamoja kuunga mkono wasaidizi wa sheria
news phpto

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(SMT) na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) zimejidhatiti kwa pamoja kuunga mkono wasaidizi wa sheria kutokana na umuhimu walionao katika kuwafikia walengwa.

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(SMT) na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) zimejidhatiti kwa pamoja kuunga mkono wasaidizi wa sheria kutokana na umuhimu walionao katika kuwafikia walengwa.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Katiba na Sheria Khamis Juma Maalim wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa wasaidizi wa sheria wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) katika ukumbi wa hotel ya Zanzibar Beach Resort nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Waziri huyo alisema Serikali mbili hizo zinawaunga mkono wasaidizi wa kisheria kutokana na njia muhimu ya kufikia maendeleo endelevu ya dunia (SDG).

Alisema ushirikiano wa wasaidizi wa kisheria katika nchi za SADC utaweza kuwasaidia wananchi wenye uwezo mdogo kupata haki yao ya msingi kutokana na matatizo wanayokumbana nayo.

“Serikali zetu mbili za SMT na SMZ imejidhatii kuhakikisha inawaunga mkono kikamilifu wasaidizi wa kisheria katika kutatua matatizo na kuwaletea mataendeleo wananchi wanyonge,”alisema.

Waziri Khamis alisema Zanzibar imefanikiwa kupitisha Sheria ya Msaada wa kisheria mwaka 2018 kutokana na umuhimu uliokuwepo wa kulizungumzia hilo kutokana na baadhi ya wananchi hawajui umuhimu wa kuwepo kwa wasaidizi hao.

Hivyo aliwaomba wananchi wa Zanzibar kuitumia Idara ya Msaada wa Kisheria kwani ipo kwa ajili yao na imejipangia mikakati ya kuwafikia wananchi wote kwa kuweka ofisi kwenye Wilaya zote ili kuwafikia wananchi wake.

Waziri Khamis amewashukuru waandaji wa mkutano huo pamoja na waliofanikisha kufanyika kutokana na umuhimu wake kwa maendeleo endelevu ya nchi na kwamba huduma za kisheria zinahitaka kumfikia kila raia.

Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Profesa Sifuni Mchome alisema mwaka 2017 SMT imepitisha sheria ya kuwatambua na kwa sasa wamesambaa nchi nzima .

Alisema tayari wasaidizi wa kisheria Tanzania Bara wanatambulika kisheria na wamekua wakitoa msaada mkubwa kwa wananchi wenye mahitaji hayo katika maeneo mbali mbali.

“Wasaidizi wa kisheria Tanzania Bara wanafanya kazi vizuri na wanatambuliwa na Serikali lakini changamoto kubwa zinazowakabili ni ukosefu wa fedha pamoja na uelewa mdogo miongoni mwa wananchi,”alifafanua.

Akizungumza kabla ya ufunguzi wa mkutano huo, Mkurugenzi wa Idara ya Msaada wa Kisheria Hanifa Ramadhan Said alisema mkutano huo umefanyika wakati muafaka kwa kubadilishana uzoefu na kuendeleza mbele huduma za kisheria kwa wananchi hususan maskini na wenye mahitaji maalum vijijini.

Mkutano huo ulitarajiwa kufanyika mwezi wa sita mwaka huu, kutokana na kuzuka kwa maradhi ya homa kali ya mapafu inayotokana na virusi vya corona na umefanyika leo ambapo baadhi ya wanachama wa shiriki wa jumuiya hiyo ambao hawajaweza kufika wanahudhuria mkutano huo kwa njia ya mtandao wa kijamii wa Zoom.

Mkutano huo umedhaminiwa na Shirika la Legal Services Facility LSF ambapo Afisa Mtendaji Mkuu , Lulu Ng'wanakilala amesema wamekuwa wakifanya kazi kwa karibu na Wizara ya Katiba na Sheria kwa Serikali zote mbili katika kuwezesha upatikanaji wa haki nchini kwa kupitia watoa huduma za msaada wa kisheria nchini, Tanzania bara na Zanzibar. Kuwezesha kufanyika mkutano huu ni mwendelezo wa dhamira ya LSF ya kuleta mapinduzi katika upatikanaji wa haki katika nchi za SADC.

Huduma za Tehama

Barua Pepe Msaada wa kisheria

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

MAHAKAMA DPP WAKFU LRC SADC IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 772, Mazizini, Zanzibar
Tel.: +255(24)2234683 Mhe Waziri



Tel.: +255 (24)2234684 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2234689
Email: info@sheriasmz.go.tz