Hits 38533 | 1 online
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumushi na Utawala Bora Mhe Haroun Ali Suleiman amewahimiza watendaji wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake wa majukumu yake ya kiutendaji.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumushi na Utawala Bora Mhe Haroun Ali Suleiman amewahimiza watendaji wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake wa majukumu yake ya kiutendaji.
Ameyasema hayo wakati alipokutana na Mwanasheria Mkuu pamoja na watendaji wa Ofisi hio pamoja na wafanyakazi ikiwa ni utaratibu wa kukutana na viongozi wa Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora mara baada ya kuapishwa.
Mhe Haroun amesema jukumu kubwa liliopo ni kuhakikisha kila mtendaji anawajibu wa kusimamia majukumu yake na kuweka mbele maslahi ya taifa ikiwemo kuwa mzalendo wa kweli , kuwa muadilifu, kujenga uaminifu na kusimamia vyema majukumu ya Serikali wakiamini Zanzibar itajengwa na wazanzibari wenyewe.
‘Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ni Taasisi kubwa hivyo watendaji hakikisheni wafanyakazi mnawasomesha , zinapokuja fursa za ndani na nje ya nchi mnawapa wafanyakazi ili waingie katika ushindani wa kitaalamu wa fani mnayoifanyia kazi masuala ya Sheria na Katiba ndio yanayoipa sura nchi na ndimo kunakonekana utawala bora kubwa Zaidi ya yote hakikisheni mnashinda kesi za Serikali hii ndio faida ya kuwa na wataalamu.
wazalendo’alisisitiza mwalimu Haruon.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt Mwinyi Talib amemuhakikishia waziri pamoja na wafanyakazi kuwa ataendelea kusimamia vyema majukumu aliyopangiwa ikiwemo maslahi yao na kuondosha manunguniko ili ufanisi uwe bora zaidi
Aidha ameahidi kuandaa mpango kazi wa miaka mitano utakaoonesha utekelezaji,uchambuzi wa bajeti na matumizi yake, majukumu ya watendaji na wafanyakazi, vitendea kazi na vyanzo vya mapato ili kukamilisha ujenzi wa jengo la Ofisi hio kwa Unguja na Pemba katika kiwanja kipya kinachotegemwa kujengwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kilichopo Tibirinzi Chake Chake
‘sambamba na hili Ofisi ya Mwanasheria Mkuu imeanza kutayarisha mpango mkakati wa miaka kumi baada ya Mpango Mkakati wake uliopo kumaliza muda ambapo rasimu ya awali imeshawasilishwa kwa mshauri elekezi wa Afisi yetu’ alisema Dkt Mwinyi
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji Mkurugenzi Mipango, Uendeshaji na Rasilimali watu Bi Hamisa Mmanga amesema kwa kipindi cha Julai hadi Septemba Ofisi ya Mwanasheria Mkuu imeandaa jumla ya kanuni 13 zinazotokana na sheria tofauti ili ziweze kutekelezeka, kuchapisha nakla 500 za Katiba ya Zanzibar 1984 pamoja na marekebisho yake hadi 2016 na kugaiwa kwa taasisi mbalimbali za Serikali ikiwemo Baraza la Wawakilishi, Baraza la Mapinduzi, Mahakama na taasisi nyengine
Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar 1964 Mwanasheria Mkuu ndio Mshauri Mkuu wa Serikali kwa mambo yote ya Kisheria.