Hits 56896 | 4 online
Mkurugenzi wa Idara ya Uandishi wa Sheria na Sera za Kisheria ndugu Saleh Said Mubarak amesema lengo la kuanzishwa kwa Jumuiya ya Mawakili Zanzibar inayojitegemea ni kuilinda Katiba ya Zanzibar, kukuza utawala wa sheria.
Mkurugenzi wa Idara ya Uandishi wa Sheria na Sera za Kisheria ndugu Saleh Said Mubarak amesema lengo la kuanzishwa kwa Jumuiya ya Mawakili Zanzibar inayojitegemea ni kuilinda Katiba ya Zanzibar, kukuza utawala wa sheria, mawakili kukidhi viwango vya mafunzo , maadili na uwezo wa kitaaluma Kuwezesha utambuzi wa mageuzi ya mfumo wa taaluma ya sheria utakaoongeza uwajibikaji na ufanisi pamoja na Kuweka utaratibu muafaka wa utoaji fursa sawa kwa mawakili wote wa Zanzibar
Mubarak ambae pia ni muwezeshaji katika semina hio amesisitiza kuwa moja kati ya vipengele muhimu katika rasimu hio ni misingi ya uongozaji wa Jumuiya ambapo ameeleza kuwa ni kuiendeleza amani, umoja na mshikamano, kulinda maslahi ya umma, sambamba na Jumuiya kutojiingiza, kutojihusisha au kufungamana na mambo ya kisiasa ya chama chochote cha siasa au mambo ya uchaguzi wa kisiasa.