Hits 56918 | 2 online
MHE WAZIRI … Tume ya kurekebisha Sheria kushirikiana na vyombo vya habari ili wananchi wapate kuifahamu.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Khamis Juma Mwalim amewaomba wahariri vyombo vya habari, waandishi na watayarishaji vipindi kutumia vyema kalamu zao na kupaza sauti zao kwa kuwa mabalozi wazuri na jukwaa la kuwapasha habari wananchi, juu ya kazi zinazofanywa na Tume ya kurekebisha sheria ili jamii iweze kuifahamu na kuielewa majukumu yake
Ameyasema hayo katika semina ya kuwajengea uelewa waandishi wa habari, watayarishaji vipindi na wahariri wa vyombo mbali mbali vya habari kuhusu majukumu na kazi za Tume ya Kurekebisha sheria iliyofanyika katika ukumbi wa Bima uliopo
Mhe Khamis amesema jamii inaviamini vyombo vya habari hivyo umakini unahitajika katika kufikisha ujumbe ulio sahihi kwa vile vyombo vya habari vina jukumu kubwa la kuelimisha jamii ‘nchi ni yetu sote tuwe wazalendo waandishi andikeni habari zenye uhalisia kwa kuzingatia maadili ya uandishi kwani taarifa zinazohusiana na masuala ya sheria zinahitaji umakini na uwelewa mzuri’alisisitiza
Aidha ameikumbusha Tume ya Kurekebisha sheria wajibu wa kukusanya maoni ya wananchi wakati wa kufanya mapitio ya marekebisho ya sheria mbali mbali wanazozifanyia kazi kabla ya kuwasilisha mapendekezo yake serikalini kwa kuwashirikisha na kuwashirikisha wanahabari ili Tume hio iweze kusikika na jamii kufahamu kile wanachokifanya.