Head image
Govt. Logo

Hits 30393 |  1 online

     
Mkurugenzi Idara ya Mswaada Kisheria Zanzibar Bi Hanifa Ramadhan Said SMZ inahakikisha wananchi wote wamepata huduma stahiki
news phpto

Mkurugenzi Idara ya Mswaada Kisheria Zanzibar Bi Hanifa Ramadhan Said SMZ inahakikisha wananchi wote wamepata huduma stahiki.

Imeelezwa kuwa azma ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar nikuahakikisha wananchi wote wanapata huduma stahiki za msaada wa sheria kutoka kwa wanasheria ambao wanasifa zinazoitajika kwa mujibu wa sheria

Mkurugenzi wa Idara ya Msaada wa Kisheria Bi Hanifa Ramadhan Said ameyasema hayo wakati alipokuwa akifunguwa mafunzo ya siku moja ya kujenga uelewa kwa wasaidizi watoaji huduma za msaada wa kisheria kutoka taasisi mbali mbali za watoa huduma kwenye ukumbi wa mkutano Wizara ya Katiba na Sheria Mazizini.

Bi Hanifa amesema kuwa kila mwananchi anayo haki ya kupata msaada wa kisheria bila ya ubaguzi kwa mujibu wa Sheria na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ambayo inasisitiza kulindwa kwa haki za binadamu

“Uwepo wa Idara ya Msaada wa Kisheria Zanzibar, kunafungua ukurasa mpya katika kuhakikisha kuanzisha haki na wajibu kwa watoaji wa msaada wa huduma za kisheria, vigezo na viwango pamoja na usimamizi mzima wa huduma za msaada wa kisheria” alisisitiza.

Mkurugenzi Hanifa ameiomba jamii kuwa tayari kuitumia Idara ya Msaada wa Kisheria pamoja na wasaidizi wake kwa utaratibu maalum uliowekwa kwani sio watu wote watapewa huduma hio isipokuwa kwa yule asie na uwezo kama sheria na kanuni zinavyoelekezwa

Aidha amesisitiza kuwa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 inatambua na inahakikisha haki na inajumuisha suala la msaada wa kisheria kama msingi wa haki za binadamu kwa watu wote hivyo ni wajibu wa watoaji wa msaada wa kisheria kuifuata miongozo iliyowekwa ili kuweza kuisaidia jamii kupata msaada wa kisheria kwa ufanisi na kwa wakati.

Huduma za Tehama

Barua Pepe Msaada wa kisheria

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

MAHAKAMA DPP WAKFU LRC SADC IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 772, Mazizini, Zanzibar
Tel.: +255(24)2234683 Mhe WaziriTel.: +255 (24)2234684 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2234689
Email: info@sheriasmz.go.tz