Hits 70228 | 2 online
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Khamis Juma Maalim amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kujenga majengo ya kisasa ya Mahakama
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Khamis Juma Maalim amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kujenga majengo ya kisasa ya Mahakama ili kuimarisha utendaji wa kazi kwa taasisi hiyo nchini.
Akizungumza baada ya utiaji saini wa ujenzi wa mahakama Kuu ya Zanzibar huko vuga amesema ujenzi wa mahakama hizo umekusudia kuwajengea uwezo watendaji katika kutekeleza Shughuli zao na kufikia lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi.
Hivyo amewataka wakandarasi kuhakikisha wanajenga jengo imara pamoja na kumaliza kwa muda ulipangwa ili kuepusha Migogoro itakayoweza kujitokeza.
Naye Jaji Mkuu wa zanzibar Omar Othuman Makungu amesema kutokana na udogo wa jengo liliopo sasa kunasababisha ucheleshwaji wa kesi hali inayoleta usumbufu kwa wananchi na Mahakimu.
Kwa upande wake Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya Advent Construction Limited inayojenga mahakama hiyo huko Tunguu Bw Ashutosh Jog amesema jengo hilo la Ghorofa nne, litahagharimu Shilingi Billioni Kumi na Sita.