Hits 56897 | 4 online
Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh Omar Othman Makungu amesema ushirikiano wa pamoja kwa nchi za Afrika utasaidia kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kuimarisha maendeleo katika bara hilo.
Akifunga mkutano mkuu wa mwaka wa jumuia ya Majaji na Mahakimu wa nchi za Afrika Mashariki huko hoteli ya Madinat-lbar Mbweni amesema nchi za Afrika zimekuwa zikitoa mchango mkubwa wa kuyatafuta ufumbuzi masuala mbali mbali ya maendeleo ya kijamii ikiwemo uwekezaji, ardhi pamoja na mazingira.
Amesema hatuwa hiyo imeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kufikiwa kwa malengo ya kuwa na uchumi endelevu unaowanufaisha wananchi wengi katika nchi hizo.
Nae raisi wa chama cha majaji tanzania Bw Wiberforce Luhwago amesema kupitia mkutano huo wamejifunza mambo mbali mbali ya sekta ya ardhi pamoja na kubadilisha uwezowefu hatua itakayosaidia kuongeza ufanisi katika utekelazaji wa kazi zao
Aidha amewapongeza wajumbe wa mkutano huo kwa ushirikiano mzuri walioonyesha na kufanikisha kuibua michango mbalimbali ya kuleta maendeleo kwa jumuia za nchi za Afrika Mashariki .
Zaidi ya washiriki 350 kutoka nchi za Afrika Mashariki wamehudhuria mkutano huo wakiwemo Majaji na Mahakimu kutoka Sudani Kusuni, Kenya, Tanzania, Rwanda na Burundi.