Head image
Govt. Logo

Hits 32643 |  1 online

     
Mwenyekiti Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar Mhe Jaji Mshibe Ali Bakari amesema talaka sio suluhisho la kutatua Migogoro ya ndoa
news phpto

Mwenyekiti Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar Mhe Jaji Mshibe Ali Bakari amesema talaka sio suluhisho la kutatua Migogoro ya ndoa

Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Mhe Jaji Mshibe Ali Bakari ameishauri jamii kutokwepa majukumu yao katika malezi ya familia ili kuondosha wimbi la migogoro katika ndoa inayosababisha talaka za mara kwa mara

Akizungumza katika mafunzo ya makaadhi wa wilaya kuhusu uendeshaji wa kesi na utoaji wa hukumu kwa misingi ya dini kiislamu amesema kitendo cha kwenda mahakamani kudai talaka sio suluhisho la kutatua kero za kufamilia bali linaongeza mivutano ya kijamii hasa kwa maelzi ya watoto

Jaji Mshibe amewaomba masheikh na walimu kubeba dhima waliyokuwa nayo kuiunganisha jamii hasa katika kutatua migogoro hiyo kwa misingii ya kimaadili ya dini na utamaduni kabla ya kuzifikisha kesi mahakamani

Akiwasilisha mada kuhusu uandishi wa hukumu Mhe Jaji Abdulhakim Ameir Issa amesema ni lazima makadhi hao kufahamu wanafanya kazi ya umma katika kuiambia jamii kuhusu uamuzi unaotokana na suala lililopo mbele yake uamuzi atakaofanya kutokana na taratibu za kisheria

Jumla ya mada mbili zilmewasilishwa ikiwemo uandishi wa hukumu na tamko la Cairo katika Mafunzo hayo yanawakutanisha Makadhi wa Wilaya kutoka Unguja na Pemba yameandaliwa na Mahakama kuu Zanzibar kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP

Huduma za Tehama

Barua Pepe Msaada wa kisheria

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

MAHAKAMA DPP WAKFU LRC SADC IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 772, Mazizini, Zanzibar
Tel.: +255(24)2234683 Mhe WaziriTel.: +255 (24)2234684 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2234689
Email: info@sheriasmz.go.tz