Head image
Govt. Logo

Hits 27688 |  2 online

     
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Khamis Juma Mwalim akitoa taarifa kwa waandishi wa wa wahabari kuhusiana na wiki ya msaada wa Kisheria katika ukumbi wa Mkutano wa Wizara ya Katiba na Sheria.
news phpto

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Khamis Juma Mwalim akitoa taarifa kwa waandishi wa wa wahabari kuhusiana na wiki ya msaada wa Kisheria katika ukumbi wa Mkutano wa Wizara ya Katiba na Sheria.

KWA mara ya kwanza Zanzibar inatarajiwa kuadhimisha wiki ya msaada wa kisheria ambayo yataenda sambamba na siku ya sheria ili kuimarisha ustawi wa jamii kupitia upatikanaji wa msaada wa kisheria.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho hayo ,Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mhe Khamis Juma Mwalim, amesema kuwa maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika Febuari saba mwaka huu ambapo Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar anatarajiwa kuwa mgeni rasmin.

Waziri Khamis amesema jamii inakabiliwa na changamoto kubwa ikiwemo ya vitendo vya udhalilishaji kiasi ambacho kinaathiri ustawi wa jamii.

Alieleza kuwa upatikanaji wa haki hasa kwa watu wasiokuwa na uwezo utapelekea kuviangamiza vitendo hivyo na kuwa na ustawi mzuri wa jamii.

Ameleza kuwa katika kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho hayo Wizara ya Katiba na Sheria imeandaa shughuli mbalimbali ikiwemo utoaji wa elimu kwa wananchi na kutembelea wait waliopo vizuizini waliopo karaoke chuo cha Mafunzo Kilimani ili kutoa msaada wa kisheria.

Aidha amesema kuwa katika maadhimisho hayo kutakuwa na uzinduzi wa mfumo wa usajili wa watoa huduma za msaada wa kisheria kwa njia ya kieletroniki na uzinduzi wa sheria ya msaada wa kisheria kwa lugha nyepesi ya Kiswahili.

“Niwaombe mushy waandishi kushirikiana nasi katika kuhakikisha wananchi wetu wanapata taarifa sahihi juu ya upatikanaji wa msaada wa kisheria katika nchi yetu”alisema.

Aidha alieleza kuwa kuna baadhi ya wananchi wanyonge haki zao zinapotea kwa sababu ya unyonge wao hivyo utoaji wa elimu utasaidia kupata haki zao.

Kuanzishwa kwa Idara ya Msaada wa Kisheria ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi katika kusimamia upatikanaji haki demokrasia na utawala bora karaoke kuona wananchi wote wanapata ufumbuzi wa matatizo yanayohusu sheria.

Waziri Khamis amekutana na waandishi wa habari katika ukumbi wa Wizara ya Katiba na Shetia ikiwa ni kuelekea wiki ya msaada wa huduma za kisheria .

Alisema moja ya changamoto iliyokuwa ikiwakabili wananchi kwa muda mrefu ni tatizo la msaada wa kisheria katika vyombo vya sheria ikiwemo Mahakama.

Alifahamisha wananchi wanakabiliwa na kesi ambazo ufumbuzi wake ni mwepesi wa kupata msaada wa kisheria lakini hakuna taasisi au Jumuiya yenye uwezo wa kufanya kazi hiyo.

''Tumeunda Idara ya huduma za msaada wa kisheria kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kupata ufumbuzi wa mashauri yao ikiwemo wafungwa waliopo Magerezani na watuhumiwa wengine''alisema.

Aidha alisema katika wiki ya siku ya huduma za msaada wa kisheria wananchi wametakiwa wajitokeza kwa wingi kupata huduma za kisheria kwa kutaja shida na changamoto mbali mbali zinazowakabili ikiwemo kesi.

''Hii ni fursa adhimu sana ambapo wananchi wanatakiwa kuitumiya kwa ajili ya kupata msaada wa kisheria katika masuala mbali mbali ikiwemo madai na mashauri yaliopo Mahakamani''alisema.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya msaada wa kisheria Hanifa Ramadhan Said Soud alisema wanatarajia kuzinduwa kitabu rasmin kuhusu mfumo wa usajili kwa watu wanaohitaji msaada wa kisheria.

''Tunataka watu wajuwe kwamba huduma za msaada wa kisheria zinapatikana bure baada ya kuanzishwa taasisi rasmin ili kuwawezesha wananchi wanyonge waweze kuwasilisha malalamiko yao''alisema.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Ndg George Joseph Kazi alisema Wizara ipo katika hatua za mwisho za kutafsiri sheria zote kwa lugha nyepeni ya Kiswahili

''Tumekubaliana na hilo wataalamu wetu wapo katika hatua za mwisho za kutafsiri sheria na maandiko mbali mbali kwa lugha nyepesi sana ili kuweza kufahamika na wananchi wengi.

Huduma za Tehama

Barua Pepe Msaada wa kisheria

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

MAHAKAMA DPP WAKFU LRC SADC IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 772, Mazizini, Zanzibar
Tel.: +255(24)2234683 Mhe Waziri



Tel.: +255 (24)2234684 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2234689
Email: info@sheriasmz.go.tz