Hits 70254 | 4 online
Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu amesema Idara ya Mahakama imejipanga kuleta mabadiliko makubwa ya kiutendaji katika miaka mitano ijayo ili kuhakikisha suala la utoaji wa haki linafanikiwa.
Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu amesema Idara ya Mahakama imejipanga kuleta mabadiliko makubwa ya kiutendaji katika miaka mitano ijayo ili kuhakikisha suala la utoaji wa haki linafanikiwa.
Akizungumza katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul Wakil Kikwajuni katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Sheria Zanzibar amesema kufanya hivyo kutawasaidia watendaji wa Mahakama hizo kufanyakazi kwa ufanisi.
Hivyo amewashauri wanasheria na mawakili wa kujitegemea kupelekea mapendekezo yao ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kusikilizwa kabla ya kuwasilisha Mahakamani.
Aidha Jaji Makungu amesema Mfumo wa Demokrasia ya vyama vingi kamwe haupaswi kuwa sababu za kuvuruga amani iliopo, akibainisha matukio kadhaa yaliojitokeza katika chaguzi zilizopita kutokana na wananchi kutotii Sheria.
naye Waziri wa Katiba na Sheria Khamis Juma Mwalimu amesema Wizara hiyo itaendelea na Jukumu la kusimamia utawala wa Sheria na upatikanaji wa haki kwa wananchi wote.